• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 2:31 PM
Familia Kilifi zashauriwa zikae pamoja maradhi ya kiakili yakiongezeka

Familia Kilifi zashauriwa zikae pamoja maradhi ya kiakili yakiongezeka

NA ALEX  KALAMA

Idara ya Afya Kaunti ya Kilifi imedokeza kuwa mwaka huu pekee, visa zaidi ya 4,000 vya maradhi ya akili vimeripotiwa, baada ya watu hao kufika hospitalini kwa matibabu.

Akizungumza mjini Kilifi, Waziri wa Afya Kilifi Peter Mwarogo amesema kuwa, baadhi ya wagonjwa hao walikuwa wanakumbwa na msongo wa mawazo, wengine wakiugua maradhi hayo kutokana na utumizi wa mihadarati.

“Hapa katika kaunti yetu ya Kilifi visa vya maradhi ya akili vinazidi kuongezeka, kuanzia mwezi Januari mwaka huu wa 2023 tumerekodi visa zaidi ya 8,000 vya watu wanaougua.

Na ukiangali baadhi ya visa hivi ambavyo tumeweza kuvirekodi ni kwamba vimechangiwa na utumizi wa mihadarati,” alisema Bw Mwarogo.

Kwa sababu hiyo, waziri huyo ameitaka jamii kuwa karibu na familia zao, ili kutambua iwapo mmoja wao anapitia hali ngumu ambazo huchangia maradhi ya hayo ya afya ya akili.

Aidha, Bw Mwarogo aliongeza kuwa, kwa sasa wamepeana mafunzo kwa madaktari wa nyanjani ili kusaidia jamii kutambua iwapo mtu anaugua maradhi ya akili na jinsi ya kukabiliana na maradhi hayo.

“Tumelipa kipaumbele suala la kupatia mafunzo madaktari wetu wa nyanjani kuhusiana na tatizo ya afya ya akili, zaidi ya vituo 125 vya afya viko na wahudumu wa afya ambao wako na ujuzi wa kuweza kusaidia watu ambao wana matatizo ya akili.

Hospitali yetu ya kaunti na pia nne za ngazi ya kaunti ndogo ziko na wataalamu wa kutosha wenye ujuzi wa utoaji huduma za dharura kwa watu wanaougua maradhi ya afya akili  hapa Kilifi,” alisema Bw Mwarogo.

  • Tags

You can share this post!

Anne Amadi aanza kujitayarisha kung’atuka kama Msajili...

Utafiti wakanusha; ‘stress’ haisababishi...

T L