• Nairobi
  • Last Updated May 6th, 2024 2:59 PM
Utafiti wakanusha; ‘stress’ haisababishi ‘mtambo’ kushindwa kunguruma

Utafiti wakanusha; ‘stress’ haisababishi ‘mtambo’ kushindwa kunguruma

NA CECIL ODONGO

WATAFITI wamebaini kuwa msongo wa mawazo na shauku (anxiety) haina uhusiano wowote na ukosefu wa nguvu za kiume kinyume na jinsi imekuwa ikifikiriwa.

Utafiti wa Wanasayansi kutoka Marekani ulihusisha wanaume ambao wameathiriwa na msongo wa mawazo au shauku. Hii ni kwa sababu kumekuwa na dhana kuwa tapo hilo ndilo mara nyingi hukosa nguvu za kiume na kutatizika katika masuala ya uzazi.

Mwanzo, wanasayansi hao walibaini kuwa wanaume walio katika hali hizo mbili hukosa kupata ashiki wakati wa mapenzi na hivyo imekuwa ikifasiriwa kuwa huenda hawana nguvu za kiume.

Hata hivyo, ilibainika kuwa wanaume ambao wana msongo wa mawazo na shauku walikuwa na viwango vya chini vya mbegu za kiume ndiposa wakati mwingine huwa vigumu kupata ashiki. Ingawa hivyo, hakukuwa na uhusiano wowote kuwa kupungua huko kwa nguvu za kiume kulisababisha mwanaume kukosa kuzalisha.

“Msongo wa mawazo huchangia kubadilika kwa homoni ambayo huathiri fikira na akili huashiria sehemu ya uzazi mwilini kukomesha mchakato wa kutengeneza mbegu za kiume. Hata hivyo, utulivu wa kiakili husababisha mbegu za kiume ziendelee kutengenezwa na hivyo hilo haliwezi kusemekana kufanya mwanaume kuwa tasa,” ukasema utafiti huo.

Watafiti hao hata hivyo, wanasema walilemewa kubaini kiwango cha homoni kwa mwanamume ambaye ana msongo wa mawazo au shauku na wanalenga kuzamia zaidi suala hilo. Kile ambacho walitilia manani ni kuwa, wanaume wanastahili kufanyiwa uchunguzi kuhusu afya ya kiakili ili kuwezesha mwili wao kuwa dhabiti katika kutengeneza mbegu za kiume.

“Kutokana na utafiti huu, ni vyema iwapo wale ambao wameathiriwa na msongo wa mawazo pamoja na shauku, wasiamini kuwa hali yao inachangia moja kwa moja wao kukosa mbegu za kiume. Dhana hii ni potovu,” watafiti wanahitimisha.

  • Tags

You can share this post!

Familia Kilifi zashauriwa zikae pamoja maradhi ya kiakili...

Malala halali: UDA wafungua ofisi mpya Kisumu kunasa...

T L