• Nairobi
  • Last Updated May 30th, 2023 10:05 AM
Fidia hutegemea idadi ya mifupa ya mfu – Wakili

Fidia hutegemea idadi ya mifupa ya mfu – Wakili

Na RICHARD MUNGUTI

WAKILI Alice Jepkoech Yano alishangaza tume ya huduma za mahakama (JSC) Ijumaa aliposema kuna jamii inayohesabu mifupa ya mhasiriwa wa mauaji kufidia familia yake idadi sawa ya mifugo.

Akihamasisha kuhusu mbinu badala za kusuluhisha mizozo, Bw Yano alisema jamii katika kaunti ya Elgeyo Marakwet huadhibu vikali wanaotekeleza mauaji.

Wakili huyo alisema fidia hii inayolipwa na wajomba wa mshukiwa imefanya jamii katika kaunti ya Elgeyo Marakwet kuogopa kutenda uhalifu wa kuua.

Wakili huyo alisema jamii katika kaunti hiyo alipohudumu kama mshauri wa masuala ya kisheria akipokea mshahara wa Sh109,000 alisema wajomba wa mshukiwa wa mauaji hufidia familia ya mhasiriwa mifugo sawa na idadi ya mifupa ya marehemu.

“Katika jamii kaunti ya Elgeyo Marakwet mmoja akiua ndugu za mama yake huhesabiwa idadi ya mifupa ya marehemu na kufidia familia yake,” alisema Bi Yano.

Mwanasheria huyo mwenye tajriba ya miaka 25 akitoa huduma ya uwakili kwa watu mbali mbali alisema “kamati za wazee katika jamii mbali mbali nchini husuluhisha mizozo mingi.”

Alieleza JSC kwamba katiba ya 2010 inatambua majopo ya kuamua kesi kwa lengo la kupunguza mrundiko aliosema umekuwa mahakamani kwa muda mrefu.

Wakili huyo alieleza tume ya huduma za mahakama JSC kwamba endapo itamteua kuwa Jaji Mkuu atahamasisha kila jamii nchini Kenya kubuni utaratibu wa kusuluhisha mizozo ya ndoa , urithi wa mali na kesi za mashamba.

Akisema amechangia kuangamiza ukeketaji wa wasichana. Pia alisema yeye na mawakili wengine waliwachangia kina mama katika Elgeyo Marakwet kuezeka nyumba zao kwa mabati.

Bi Yano ambaye ni mjane alieleza JSC kuwa hapingi kuteuliwa kwa mwanamke kuwa Jaji licha ya vitengo vingi katika idara ya mahakama kusimamiwa na wanawake.

Wakili huyo alihojiwa kaimu Jaji Mkuu Philomena Mwilu kuhusu mbinu atakazoimbua kufanikisha utenda kazi katika idara ya mahakama.

Akijibu alisema atatumia ujuzi aliopata katika tume ya kubadili katiba chini ya uongozi wa Prof Pal Yash Ghai kuzindua mbinu mpya za kuimarisha utenda kazi katika sekta zote za idara ya mahakama.

Lakini wakili huyo alishindwa kujibu maswali mengi kuhusu ufisadi, uzoefu katika masuala nyetu ya sheria n ahata kusuluhisha kesi za dhuluma za kimapenzi katika mahala pa kazi.

  • Tags

You can share this post!

GSU na KPA wako kikaangoni voliboli ya Afrika ya wanaume...

‘Simu ya mwenzako sumu’