• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 10:15 PM
GSU na KPA wako kikaangoni voliboli ya Afrika ya wanaume ikiingia robo-fainali leo

GSU na KPA wako kikaangoni voliboli ya Afrika ya wanaume ikiingia robo-fainali leo

Na GEOFFREY ANENE

WAWAKILISHI wa Kenya kwenye mashindano ya Afrika ya volivoli ya wanaume, GSU na KPA wanarejea uwanjani kwa mechi za robo-fainali wakihitaji miujiza kutinga nusu-fainali mjini Tunis, Tunisia leo Ijumaa.

KPA itakuwa ya kwanza kushuka uwanjani saa nane mchana saa za Kenya kupepetana na mabingwa wa mwaka 1984, 1987, 2008, 2009 na 2012 Zamalek. Wamisri hao pia wanajivunia kushinda Ligi Kuu nchini mwao mara 26.

Vijana wa kocha Sammy Mulinge wanashiriki mashindano haya kwa mara ya kwanza kabisa. Hawajawahi kushinda Ligi Kuu ya Kenya. Walipata tiketi ya kushiriki dimba hili baada ya kukamilisha Ligi Kuu ya msimu 2019 katika nafasi ya pili nyuma ya GSU. Ligi haikufanyika mwaka 2020 kutokana na mkurupuko wa virusi vya corona.

Katika mahojiano ya awali, Mulinge alisema KPA itajikakamua vilivyo kutafuta ushindi dhidi ya Zamalek ambayo ni moja ya timu zinazopigiwa upatu kutwaa ufalme wa kombe hili.

GSU itavaana na mabingwa wa mwaka 1994, 1998, 2000 na 2014 Esperance ambao ndio washindi wa Tunisia na wanajivunia mataji 21 ligini mwao. Vijana wa kocha Gideon Tarus wana uzoefu wa miaka mingi ikiwemo kutwaa nishani ya shaba mwaka 2005 nchini Benin.

Ratiba ya leo (Aprili 23): Saa nane mchana – Swehly (Libya) na Nemostar (Uganda), Zamalek (Misri) na KPA (Kenya); Saa kumi jioni – Kelibia (Tunisia) na Port Douala (Cameroon); Saa kumi na mbili jioni – Esperance (Tunisia) na GSU (Kenya).

  • Tags

You can share this post!

Mwaniaji kiti cha ubunge Juja kupandishwa kizimbani Aprili...

Fidia hutegemea idadi ya mifupa ya mfu – Wakili