• Nairobi
  • Last Updated May 12th, 2024 5:17 PM
Hospitali yakiri kulemewa na wagonjwa wa corona

Hospitali yakiri kulemewa na wagonjwa wa corona

Na CHARLES WASONGA

HOSPITALI ya Mafunzo, Utafiti na Rufaa ya Chuo Kikuu cha Kenyatta (KUTRRH) imetangaza kuwa imelemewa na idadi kubwa ya wagonjwa wa corona.

Kwenye taarifa kwa wauguzi wa hospitali hiyo, mkurugenzi wa kitengo cha uuguzi Edward Omondi pia amewaagiza wauguzi walioko likizoni kurejea kazini mara moja kukabiliana na hali hiyo.

Vile vile, amewaagiza wale walioko kazini kuendelea kuhudumu hata siku zao za mapumziko akiahiadi kuwa watafidiwa siku hizo “hali ya kawaida itakaporejelewa.”

“Hospitali hii inalemewa na ongezeko kubwa la wagonjwa wa Covid-19 kufuatia ongezeko la visa vya maambukizi nchini. Wodi za kutenga wagonjwa zimejaa sawa na vitengo vingine vya kuwahudumia wagonjwa wanaohitaji huduma za dharura,” akasema Bw Omondi.

“Hii ndio maana hospitali inapanga kuajiri wauguzi zaidi na wahudumu katika vitengo vingine. Hii ni kwa sababu ni sera yetu kutowakataa wagonjwa kwani Wakenya wanahitaji vitanda na huduma,” akaongeza.

Bw Omondi pia alisema usimamizi wa hospitali hiyo ya KUTRH unawataka wahudumu wa vitengo mbalimbali katika hospitali hiyo kuwa tayari kuhamishiwa vitengo vingine “kulingana na mahitaji ya hospitali hii.”

Hospitali ya KUTRRH ni mojawapo ya hospitali chache za umma nchini zenye uwezo wa kuwashughulikia wagonjwa wa corona.

Ndiyo hospitali yenye idadi kubwa ya vitanda, vifaa na wahudumu waliohitimu.

Hospitali nyingine zenye uwezo sawa na huo ni Hospitali Kuu ya Kenyatta (KNH), Hospitali ya Mafunzo na Rufaa ya Moi (MTRH) na Hospitali ya Mbagathi.

Hatua hiyo ya KUTRRH inajiri wakati idadi ya watu wanaofariki nchini kutokana na aina mpya ya corona maarufu kama ‘Delta’.

You can share this post!

Ndugu waliouawa na polisi wazikwa wengine wanne wakiuawa...

Pigo KCB viongozi Tusker wakifungua mwanya wa alama tatu...