• Nairobi
  • Last Updated May 9th, 2024 6:40 PM
Itumbi akata rufaa kupinga kuharamishwa kwa nyadhifa 50 za CASs

Itumbi akata rufaa kupinga kuharamishwa kwa nyadhifa 50 za CASs

NA RICHARD MUNGUTI

MTALAAMU wa masuala ya kidijitali Dennis Itumbi amekata rufaa kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu kuharamisha nyadhifa za mawaziri wasaidizi (CASs) 50 mnamo Julai 3, 2023.

Bw Itumbi aliyekuwa ameteuliwa Waziri Msaidizi katika Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia (ICT) amesema uamuzi huo wa kuwatimua kazini CASs 50 uliwaathiri pakubwa.

Bw Itumbi ameomba Mahakama ya Rufaa ibatilishe uamuzi huo wa majaji Kanyi Kimondo, Hedwiq Ong’udi na Alnashir Visram ulioharamisha nyadhifa hizo.

Majaji hao walisema Rais William Ruto hana mamlaka ya kubuni nyadhifa za kazi.

“Uteuzi wa nyadhifa 50 za CASs na Rais William Ruto unakinzana na Katiba,” majaji hao walisema.

Baada ya kusema hayo, majaji hao waliamua, “hatuna budi kuharamisha na kufutilia mbali nyadhifa hizi.”

Itumbi amelalamika kwamba uamuzi huo ulimwathiri kwa vile hawezi kuajiriwa kazi nyingine baada ya kuteuliwa na Rais Ruto kuwa Naibu Waziri.

Kupitia kwa wakili Dkt Andrian Kamotho, Bw Itumbi amesema kuwa uamuzi huo wa Mahakama Kuu ulimnyang’anya mamlaka Rais Ruto aliopewa na Kifungu 132 (4) (a) ya kubuni nyadhifa za kazi kwa ushauri wa Tume ya Kuajiri Watumishi wa Umma (PSC).

  • Tags

You can share this post!

Nyeri yajiunga na maandamano ya Azimio

Maandamano ya Azimio: Mathare, ni mguu niponye waandamanaji...

T L