• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 8:55 PM
Kagure akanusha madai ya kughushi hati ya ardhi

Kagure akanusha madai ya kughushi hati ya ardhi

NA RICHARD MUNGUTI

MWANIAJI wa kiti cha Ugavana kaunti ya Nairobi Agnes Kagure anatuhumiwa kughushi stakabadhi za umiliki wa mali ya raia wa Uingereza marehemu Roger Robson ya Sh500 milioni.

Wakili David Michuki alimweleza Jaji Maureen Odero kwamba Robson alikuwa mgonjwa kiasi cha kutoweza kutia saini stakabadhi za mali yake.

“Hadi alipoaga dunia 2012, Robson alikuwa mgonjwa mno. Asingetia saini hati yoyote,” Bw Michuki alimweleza Jaji Odero.

Jaji huyo alifahamishwa kuwa saini katika hati alizokuwa nazo Kagure zilikuwa ghushi.

Hata hivyo Bi Kagure alisisitizia mahakama kuwa ndiye mmiliki wa shamba husika.

Amesema aliuziwa na Robson kwa bei ya Sh100 milioni mwaka wa 2011.

Katika kesi aliyomshtaki wakili Guy Spencer Elms, Kagure anadai wakili huyo (Spencer) alighushi sahihi ya marehemu.

You can share this post!

Serikali ina mikakati ya kupunguza bei za mafuta –...

Mhadhiri atoa jasho Keter kinyang’anyiro cha ugavana...

T L