• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 5:50 AM
Kamishna atishia kufunga baa zinazokiuka kanuni za kuzuia virusi

Kamishna atishia kufunga baa zinazokiuka kanuni za kuzuia virusi

NA PIUS MAUNDU

KAMISHINA wa Kaunti ya Makueni, Maalim Mohammed amewaonya wamiliki 39 wa baa ambao wanakiuka kafyu na kupuuza kanuni za kuzuia kuenea kwa virusi vya corona kuwa watanyakwa na baa zao kufungwa.

Bw Mohammed alisema wamiliki wa baa hizo wamekuwa wakiendelea na tabia hiyo licha ya kuonywa mara kadhaa.

Baa hizo 39 kati ya nyingine 4,000 zimekuwa zikiendelea na biashara ya kuuza vileo baada ya muda uliowekwa wa saa moja usiku.

“Kuna mabaa ambayo yatafungwa kwa kukosa kuzingatia masharti ya kuzuia kuenea kwa virusi vya corona. Iwapo wataendelea na tabia hii basi hatutakuwa na budi ila kuhakikisha sheria inafuatwa,” akasema Bw Mohammed akiwa mjini Wote.

Baa 14 kati ya idadi hiyo zinapatikana Makueni, huku saba zikipatikana Nzaui na Mukaa kila moja, Mbooni Magharibi (4), Kibwezi (3), Makindu (2) huku Kathonzweni na Mbooni pakiwa na moja moja.

Wakati huo huo, Bw Mohammed alisema maambukizi ya virusi vya corona yanaendelea kupanda katika kaunti hiyo na akatoa wito kwa raia wajihadhari na kuzingatia masharti yaliyowekwa na serikali.

You can share this post!

Gavana atoa onyo haitakuwa rahisi kumuondoa 2022

Matumaini ya kufufuka kwa Mumias yaimarika