• Nairobi
  • Last Updated May 9th, 2024 2:36 PM
Kananu gavana wa 4 wa kike, Sonko akila hu kortini

Kananu gavana wa 4 wa kike, Sonko akila hu kortini

Bi Anne Kananu atakuwa gavana wa nne mwanamke baada ya mahakama kuu kuidhinisha uteuzi wake na bunge la Kaunti ya Nairobi.

Magavana wengine wanawake ni Charity Ngilu (Kitui), Anne Waiguru (Kirinyaga) na Joyce Laboso (marehemu) aliyekuwa gavana wa Bomet.Kufuatia uamuzi wa mahakama kuu jana, sasa ndoto ya aliyekuwa Gavana Mike Sonko kurudi afisini imeambulia patupu.

Mahakama kuu sasa imeratibisha rasmi kung’atuliwa kwa Bw Sonko kuwa gavana wa Kaunti ya Nairobi.Majaji Said Juma Chitembwe, Weldon Korir na Wilfrida Okwany walisema sheria na katiba zilifuatwa katika harakati ya bunge la Seneti na bunge la Kaunti ya Nairobi kumfukuza kazini Bw Sonko.Majaji hao walisema utaratibu uliofuatwa haukuwa na dosari.

“Kutimuliwa kwa Bw Sonko afisini kulifanywa kulingana na utaratibu uliowekwa na sheria,” walisema majaji hao huku hatima ya Sonko ikiamuliwa rasmi.“Utimuliwaji wa Bw Sonko kuwa Gavana wa Nairobi ulikuwa halali na kwa mujibu wa sheria na utaratibu uliowekwa na Katiba,” walisema majaji hao.

Majaji Chitembwe, Korir na Okwany walipuuzilia mbali madai ya Bw Sonko kwamba umma haukushirikishwa kutoa maoni kabla ya uamuzi wa kumng’atua afisini kufikiwa. Walisema tangazo lilichapishwa katika magazeti na umma kualikuwa kutoa maoni.

Majaji hao walisema bunge la Kaunti ya Nairobi lilijadili kwa mapana na marefu madai ya utovu wa nidhamu na ufisadi dhidi ya Sonko kabla ya kufikia uamuzi kuwa kulikuwa na ushahidi wa kutosha kupendekezea Seneti imfukuze kazini.

Mahakama ilitupilia mbali malalamishi ya Bw Sonko kwamba Spika wa bunge la Kaunti ya Nairobi, Bw Benson Mutura hakuwa na mamlaka ya kumteua Bi Kananu kuhudumu kama naibu wa gavana. Majaji hao walisema kama kaimu gavana, Bw Mutura alikuwa na mamlaka kisheria kumteua Bi Kananu kuhudumu.

Punde tu alipomteua Bw Mutura alikoma kutekeleza majukumu ya Gavana na Bi Kananu akaapishwa kuwa Gavana.Mbali na Bw Sonko kulikuwa na walalamishi wengine waliounga mkono kesi kwamba uteuzi wa Bi Kananu haukuwa halali kwa vile “hakukuwa na Gavana afisini ambaye angeliidhinisha uteuzi wake.

”Pia walisema Bi Kananu hakushiriki katika uchaguzi mkuu wa 2017 kama naibu wa Bw Sonko aliyemshinda Dkt Evans Kidero kwa wingi wa kura na kutangazwa gavana wa kaunti hii nambari 47.Bi Kananu aliteuliwa kuwa naibu wa Gavana na Bw Sonko kufuatia kujiuzulu kwa Polycap Igathe.

Uteuzi huu wa Bi Kananu ulipingwa katika mahakama kuu lakini kesi hiyo ikaondolewa na uteuzi wake ukajadiliwa na bunge la kaunti ya Nairobi.Bw Sonko alipinga idadi ya MCAs waliopiga kura ya kumtimua afisini akidai aliandamana na 57 ziarani Kilifi.

Majaji hao walisema wengi wa MCAs walipiga kura kumtimua.Mahakama ilisema kuwa bunge la kaunti ilimkagua ipasavyo Bi Kananu kabla ya kuwasilisha jina lake kuidhinishwa na Bw Mutura , aliyekuwa Gavana mwandamizi wa kaunti ya Nairobi.Sasa Bi Kananu atatekeleza majukumu ya Gavana

  • Tags

You can share this post!

Ni makosa kulazimishia Wakenya vyama vya kisiasa

Ogier huyo! aongoza timu ya Toyota kunyakua nafasi za kwanza