• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 4:55 PM
Kaunti zaanza kupeana chanjo

Kaunti zaanza kupeana chanjo

SIMON CIURI na GEORGE ODIWUOR

KAUNTI mbalimbali nchini zimeanza kupeana chanjo za kuepusha maambukizi dhidi ya virusi vya corona.

Jumatatu, Kaunti ya Kiambu ilianza utaratibu wa kuwapa chanjo wahudumu wake wa afya.

Afisa Mkuu wa Afya katika Kaunti hiyo, Dkt Patrick Nyaga, alisema Kaunti ilipokea dozi 13,500 za chanjo hiyo na inatarajia kumaliza zoezi hilo katika muda wa siku mbili.

Hata hivyo, alisema hilo litalingana na idadi ya watu watakaojitokeza kuchanjwa.

Dozi hizo ni sehemu ya chanjo zaidi ya milioni moja aina ya AstraZeneca ambazo zilisafirishwa nchini wiki iliyopita.

Dkt Nyaga ndiye alikuwa mtu wa kwanza katika kaunti kupewa chanjo hiyo katika Hospitali ya Thika Level Five.

Katika kaunti ya Homa Bay, zoezi hilo lilizinduliwa na Waziri wa Afya katika Kaunti, Prof Richard Muga. Waziri huyo ndiye alikuwa mtu wa kwanza kupokea chanjo hiyo.

Kaunti hiyo ilipokea dozi 9,000 za chanjo hiyo.

You can share this post!

Kenya yavuma kwa ulanguzi wa pesa

Wanasiasa waanza kushtakiwa kwa vurugu chaguzini