• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 8:55 PM
Kesi ya mauaji ya Sharon kuanza rasmi, DPP asema

Kesi ya mauaji ya Sharon kuanza rasmi, DPP asema

Na RUTH MBULA

AFISI ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (ODPP) hatimaye imetoa tarehe ya kusikilizwa kwa kesi ya mauaji ya Bi Sharon Otieno, aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Rongo.

Bi Otieno alikuwa mpenzi wa Gavana Okoth Obado wa Migori, na alipatikana ameuawa kikatili mnamo Septemba 3, 2018 akiwa mjamzito.

Upande wa mashtaka umewaorodhesha mashahidi 37 kwenye kesi hiyo ambapo Bw Obado ndiye mshukiwa mkuu.

Wengine walioshtakiwa pamoja naye ni Bw Michael Oyamo na Bw Caspal Obiero, wanaohudumu kama wasaidizi wake.

Kesi hiyo ilikosa kuanza baada ya DPP kutaja masharti ya kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona kama kikwazo kikuu.

Kesi hiyo imecheleweshwa kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Tangazo hilo linaonekana kama afueni kubwa kwa wazazi wa Sharon, baada yao kulalamika kesi hiyo ilikuwa ikichelewa sana kabla ya kuanza. Walikuwa wameomba washukiwa hao watatu kukabiliwa kisheria.

Taifa Leo imebaini kuwa Bw Obado atarejea mahakamani mwezi Julai kuhusu kesi hiyo.

Mwanafunzi huyo alipatikana ameuawa kikatili na mwili wake kutupwa msituni katika eneo la Oyugis, Kaunti ya Homa Bay.

Hapo Ijumaa, afisi ilisema kesi hiyo ilikuwa imepangiwa kuanza Machi 16 ama 17 mwaka uliopita, lakini ikaratibiwa upya baada ya Idara ya Mahakama kupunguza shughuli zake ili kudhibiti maambukizi ya corona. Hatua hiyo ilifuatia maagizo yaliyotolewa na aliyekuwa Jaji Mkuu David Maraga, kwa mahakama nchini kupunguza shughuli zake ama kuendesha baadhi ya kesi kwa njia ya mtandao.

“Awali, kesi hiyo ilikuwa imepangiwa kuanza Machi 16, 2020. Hata hivyo, iliahirishwa kutokana na masharti ya kudhibiti corona. Vikao vyake vitaanza Julai 5 na kuendelea hadi Julai 15 mwaka huu,” ikasema afisi hiyo kwenye ujumbe katika mtandao wa Twitter.

Hapo jana, wazaziwe Sharon, Bw Douglas Otieno na Bi Melinda Auma, walisema ijapokuwa kuna ripoti kuhusu kesi hiyo kuanza kusikilizwa, hawajafahamishwa rasmi.

Hata hivyo, walisema ingawa mahakama imechelewesha kesi hiyo, wana imani hatimaye watapata haki kwa mwanao.

“Hebu tungoje. Ni karibu miaka mitatu sasa tangu mtoto wetu na mwanawe ambaye hakuwa amezaliwa wauawe kikatili. Tunatarajia hatimaye atapata haki,” akasema Bw Otieno.

, ambaye hakutaka kueleza sana kutokana hali yake mbaya kiafya.

Kwenye hafla ya kukumbuka kifo chake mnamo Septemba 4 mwaka uliopita, familia hiyo ilisema maisha yao yalichukua mkondo mpya baada ya mauaji hayo.

You can share this post!

Moi sasa aweka mikakati imara kutua Ikulu 2022

Mwili wa Philip kuhamishiwa makaburi ya kifalme baadaye