• Nairobi
  • Last Updated May 9th, 2024 1:42 PM
Kiini cha 154,524 kutaka nafasi Nanyuki School

Kiini cha 154,524 kutaka nafasi Nanyuki School

Na REGINAH KINOGU

WATAHINIWA zaidi ya 150,000 walitaka kujiunga na Nanyuki School kutokana na matokeo yake bora na mafunzo ya kiufundi inayozingatia.

Matokeo mazuri ya shule hiyo kwa miaka minne iliyopita pamoja na kuanzishwa kwa masomo ya kiufundi kumefanya shule hiyo iliyoko mjini Nanyuki kuvutia maombi kutoka kwa watahiniwa 154,524.Hii imeifanya kuwa shule inayopendwa sana nchini.

Zoezi la kuchagua wanafunzi wa kujiunga na kidato cha kwanza lilipoanza, waziri wa elimu George Magoha alitangaza kuwa zaidi ya 154,000 walikuwa wameomba nafasi 384 katika shule moja.Shule hiyo ina uwezo wa kuwa na wanafunzi wasiozidi 1,000.

Wanafunzi na walimu wa shule hiyo huzingatia mpangilio mkali wa masomo ambao umedumu kwa miaka mingi. Naibu Mwalimu Mkuu Gitonga King’ori anasema kwamba mpangilio huo umetajwa kuwa sababu ya shule hiyo kufanya vyema kwenye KCSE katika miaka minne iliyopita.

Wanafunzi huwa kwenye darasa kuanzia saa kumi na siku hukamilika saa tatu na nusu jioni.Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Bw Oliver Minishi anasema wanafunzi husimamia shughuli zao nyingi kwa uelekezi wa walimu hatua ambayo anasema inawafanya kujiamini na kuwawezesha kusoma kwa bidii.

“Tumewafanya wanafunzi kumiliki shughuli za gwaride na ndio huwa wanazungumza sana. Jumatatu wiki hii ni wanafunzi wa somo la jiografia waliowasilisha mada kuhusu kulipuka kwa volkeno. Tunataka kupalilia masomo katika kila shughuli,” alisema Bw Minishi.

Kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi, wanafunzi huwa na walimu. Walimu huwa wanamaliza mtaala muhula wa kwanza wa mwaka wa mwisho na hii huwapatia wanafunzi muda wa kujiandaa kwa mtihani wa KCSE.“Tunalenga masomo na mitihani.

Hii inamaanisha kwamba tunawaambia tutawapa mtihani kuhusu masomo ya kidato fulani na wanajiandaa kwa masomo hayo na ndiyo tunatoa mtihani,” asema Bw King’ori.Shule hiyo ambayo imekuwa ikiandikisha matokeo bora kuanzia 2018 imeanzisha masomo ya kiufundi.

Inafunza taaluma kama Umeme, Useremala, Kilimo, Kompyuta na Kifaransa na imewapa wanafunzi uhuru wa kuchagua wanayotaka ili kukumbatia mtaala mpya wa kutambua uwezo wa kila mmoja (CBC).Kila mwanafunzi wa kidato cha kwanza huchagua somo moja la kiufundi analozingatia hadi kidato cha nne au wakati wa kuchagua masomo akiwa kidato cha pili.

  • Tags

You can share this post!

Makanisa yatoa onyo kuhusu ghasia 2022

Haji asihofie ugumu wakazi, aendelee kujitahidi