• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 3:31 PM
Kikosi cha Uganda chawasili kwa mechi ya kufuzu kushiriki Kombe la Dunia dhidi ya Junior Harambee Starlets

Kikosi cha Uganda chawasili kwa mechi ya kufuzu kushiriki Kombe la Dunia dhidi ya Junior Harambee Starlets

Na GEOFFREY ANENE

TIMU ya soka ya kina dada ya Uganda ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 20 imewasili jijini Nairobi kwa mechi dhidi ya wenyeji Junior Harambee Starlets ya kufuzu kushiriki Kombe la Dunia 2022.

Vipusa wa kocha Ayub Khalifan Kiyingi walifanya mazoezi yao ya mwisho ugani Phillip Omondi nchini mwao mnamo Jumatano alasiri kabla ya kuabiri ndege ya kuja Nairobi saa kumi na mbili asubuhi Alhamisi.

Timu hiyo, ambayo itakabiliana na Kenya katika mechi ya mkondo wa kwanza hapo Septemba 25, ina wachezaji watatu kutoka mabingwa wa Ligi Kuu ya Uganda Lady Doves waliokuwa Nairobi wiki chache zilizopita kwa mashindano ya Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) ya kuingia Klabu Bingwa Afrika.

Wachezaji hao ni kipa Daphine Nyayenga, beki Halima Kanyago na mshambuliaji Joweria Nagadya.

“Nadhani kikosi nilichochagua kinajumuisha wachezaji wazuri walio na uwezo wa kutufanyia kazi,” Kiyingi alieleza Shirikisho la Soka Uganda (FUFA). Kenya inayotiwa makali na kocha Charles Okere, itaelekea jijini Kampala kwa mechi ya marudiano itakayochezwa Oktoba 8. Mshindi baada ya mikondo yote miwili atamenyana na mshindi kati ya Msumbiji na Afrika Kusini katika raundi ijayo.

Wakati huo huo, Kenya imeimarisha mazoezi yake jijini Nairobi ya mchuano huo muhimu.

Kikosi cha Uganda:

Makipa – Daphine Nyayenga (Lady Doves), Joan Namusisi (Kampala Queens);

Mabeki – Sumayah Komuntale (Tooro Queens), Grace Aluka (Olila High), Biira Nadunga (Olila High), Samalie Nakacwa (Kawempe Muslim), Halima Kanyago (Lady Doves), Aisha Nantongo (Kawempe Muslim Ladies);

Viungo – Shamirah Nalugya (Kawempe Muslim Ladies), Shakirah Nyinagahirwa (Kawempe Muslim Ladies), Zaina Nandede (Kataka SHE), Catherine Nagadya (Uganda Martyrs High), Margaret Kunihira (Kawempe Muslim Ladies), Kevin Nakacwa (Uganda Martyrs High), Zaituni Namaganda (Taggy High);

Washambuliaji – Fauzia Najjemba (Kampala Queens), Hadijah Nandago (Kawempe Muslim Ladies), Juliet Nalukenge (Apollon Ladies), Joweria Nagadya (Lady Doves) na Eva Naggayi (Rines SS).

  • Tags

You can share this post!

Watoto wa demu wadharau sponsa

Mke amhadaa mumewe kuwa alitekwa