• Nairobi
  • Last Updated May 10th, 2024 5:50 AM
Kitengo cha matibabu cha Uhuru Kenyatta Wing chazinduliwa Ruiru

Kitengo cha matibabu cha Uhuru Kenyatta Wing chazinduliwa Ruiru

Na LAWRENCE ONGARO

HOSPITALI ya Ruiru Level 4 tayari imezindua kitengo kiitwacho Uhuru Kenyatta Wing ambacho Gavana wa Kaunti ya Kiambu Dkt James Nyoro alisema kina vitanda 150.

Gavana huyo alieleza kuwa kutokana na idadi kubwa ya watu katika kaunti ndogo ya Ruiru, hospitali hiyo itaweza kujisimamia hasa katika maswala ya matibabu.

Kwa wakati huu, hospitali hiyo ina wauguzi wapatao 200 na madaktari wa kutosha ambao wataweza kuwahudumia wagonjwa watakaofika huko kupokea matibabu.

Alieleza kuwa kwa muda wa miaka miwili, huduma za matibabu zimeimarika vilivyo katika kaunti ya Kiambu.

Afisa mkuu wa maswala ya afya katika kaunti Dkt Patrick Nyagah, alisema ifikapo mwezi Agosti, hospitali ya Ruiru itajisimamia yenyewe ambapo itaweza kutekeleza huduma 400 za upasuaji kwa mwezi baada ya madaktari wa kutosha kuletwa.

Alieleza kuwa kaunti ya Kiambu itaweka bohari kubwa la kuhifadhi dawa.

“Tutahakikisha kila kitu kinatekelezwa kupitia mtandao wa kidijitali ili kuhakikisha hakuna dawa inayopotea kiholela,” alifafanua Dkt Nyagha.

Naye Dkt Nyoro alieleza hospitali ya Tigoni imepiga hatua kubwa hasa wakati wagonjwa wengi wa Covid-19 walipopelekwa huko.

Alieleza kuwa tayari kuna vitanda 330 spesheli vya wagonjwa wa Covid-19 na hivi karibuni itapandishwa kuwa katika kiwango cha Level 4.

Alieleza kuwa hospitali nyingine ya Wangige ina vitanda 200 na itafunguliwa hivi karibuni kwa huduma kamili.

Mbunge wa Ruiru Bw Simon King’ara alipongeza juhudi za gavana kupandisha hadhi hospitali ya Ruiru ambayo itaweza kuhudumia idadi kubwa ya wakazi.

Alisema hadi wakati huu kaunti ndogo ya Ruiru ina idadi ya watu laki sita huku ikiwa imepata maendeleo mengi chini ya miaka mitano.

Alisema tayari mji wa Ruiru una mahakama na pia majaji watano.

Alieleza hivi karibuni kituo cha Huduma Centre kitafunguliwa ili wakazi wapate huduma ya karibu.

Alieleza pia kuwa maswala ya mashamba alifanikiwa kurekebisha baada ya afisi ya masuala ya ardhi kutatua shida za mashamba kwa miezi mitatu mfululizo mwaka wa 2020.

Alieleza kuwa mji wa Ruiru umepiga hatua kutokana na barabara kuu ya Thika Superhighway, na pia uwepo wa viwanda vingi.

  • Tags

You can share this post!

Ecowas yawashinikiza wanajeshi nchini Mali

Waathiriwa wa moto kusubiri zaidi kujengewa makazi

T L