• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 9:01 PM
Kizimbani kuhusu ulaghai wa mboga ya Sh40,000

Kizimbani kuhusu ulaghai wa mboga ya Sh40,000

Na RICHARD MUNGUTI

MSHUKIWA wa ulaghai alikana kupokea mboga na matunda yenye thamani ya Sh40,000 akitumia ujanja.

Bw Alex Oyula Baraza alidaiwa alipokea mboga na matunda haya katika soko la Wakulima mnamo Machi 12,2021 kutoka kwa wafanyabiashara kadha.

Oyula aliyekana mashtaka dhidi yake alimweleza hakimu mkuu Heston Nyaga kwamba aliwekwa rumande katika kituo cha polisi cha Kamkunji kwa siku tano kabla ya kufikishwa kortini.

Alilalamika kwamba jina lake halikuandikwa katika kitabu cha matukio (OB) licha ya kukamatwa Jumatatu wiki iliyopita.

Alimweleza hakimu ijapokuwa imenakiliwa katika cheti cha mashtaka alikamatwa Machi 12,2021 , huo.

Oyula alidai mahakamani kuwa alikamatwa Jumatatu na kuzuiliwa katika seli moja akiwa peke.

Akiwa mle , alieleza korti alikuwa anaitishwa hongo ya Sh20,000.

“Sikuwa na pesa hizo.Polisi wanieleza niwasiliane na watu wangu wa waongezee pesa hizo zitimie Sh20,000,” alisema Oyula.

Mshtakiwa alidai jina lake halikuwekwa katika OB licha ya cheti cha mashtaka kuonyesha alikamatwa Machi 12,2021.

Madai hayo ya Oyula yaliungwa mkono na mshukiwa mwingine aliyemweleza hakimu alimpata (oyula) rumande Alhamisi wiki iliyopita alipowekwa korokoroni mwendo wa saa moja jioni.

Afisa anayechunguza kesi hiyo alieleza korti hajui iwapo mshtakiwa alikamatwa Jumatatu kwa vile cheti cha mashtaka chaonyesha mshukiwa alitiwa nguvuni mnamo Machi 12,2021.

Katika mojwapo ya mashtaka hayo Oyula ameshtakiwa alipokea kwa njia ya undanganyifu kilo 110 za viazi tamu zenye thamani ya Sh5,500 kutoka kwa Judith Ouma akidai atamlipa.

Pia alikabiliwa na shtaka lingine la kupokea ndoo 10 za viazi zenye thamani ya Sh7000 kutoka kwa Bi Ann Wangechi siku hiyo hiyo ya Machi 12,2021.

Pia anakabiliwa na shtaka la kupokea viazi vingine vyenye thamani ya Sh19,000 na tikiti maji za Sh6,400 zote za thamani ya Sh25,400 kutoka kwa Bw Maxwell Kyalo akidai alikuwa na uwezo wa kuzilipa.

Pia alikana alipokea magunia mawili ya machungwa yenye thamani ya Sh6000 kutoka kwa Bw Peter Daudi.

Alikanusha mashtaka yote na kesi ikaoorodheshwa kutajwa Machi 29,2021 afisa anayeichunguza kesi dhidi yake kueleza korti ikiwa mshtakiwa alizuiliwa kwa wiki moja akiitishwa hongo ya Sh20,000..

Bw Nyaga alimweleza afisa anayechunguza kesi hiyo kuwa madai hayo ni makali na kumshauri wakili anayemtetea Oyula awasiliane na vitengo vinavyohusika kushughulikia madai hayo.

  • Tags

You can share this post!

Man-United yadengua Granada Europa League

Barcelona wapepeta Bilbao na kutwaa taji la Copa del Rey