• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 12:48 PM
Wanaume hutumia muda mwingi kuchakura mitandao, kushiriki shughuli za kujipenda, utafiti wabaini

Wanaume hutumia muda mwingi kuchakura mitandao, kushiriki shughuli za kujipenda, utafiti wabaini

NA MERCY KOSKEI

WANAUME hutumia muda mwingi kuchakura mitandaoni kuliko wanawake, Ripoti ya Matumizi ya Muda, ya Shirika la Kitaifa la Takwimu (KNBS) imesema.

Katika ripoti iliyotolewa Oktoba 18, 2023 jijini Nairobi na ofisi ya KNBS, ilionyesha kuwa wanaume hutumia muda mwingi kwenye kazi zisizo na tija kuliko wanawake.

Kulingana na KNBS, wanaume pia hutumia muda wao mwingi kwenye shughuli za kujitunza kuliko wanawake.

Watafiti hao walitaka kujua jinsi wanaume na wanawake hutumia muda wao kila siku.

Na wakabaini kuwa wanawake wanatumia muda mwingi kufanya kazi bila malipo ikilinganishwa na wanaume.

Wanawake hutumia saa nne na dakika 30 kufanya kazi zisizo na malipo, ikiwa ni pamoja na kazi za nyumbani kwa siku huku wanaume wakitumia takriban dakika 54 tu.

Kitaifa, wanawake wanatumia takriban muda zaidi kwenye kazi zisizolipwa (asilimia 2.4) kuliko wanaume (asilimia 0.4), kwenye kazi za nyumbani zisizolipwa kuliko wenzao wa kiume.

“Wanawake hutumia takriban saa tano kwa siku kwa kazi isiyo na malipo, ambayo ni takriban mara tano zaidi ya muda ambao wanaume hutumia katika kazi zisizolipwa,” ilisema ripoti hiyo.

Katika ngazi ya kaunti, mzigo wa kazi ni mkubwa zaidi kwa wanawake, wakiongozwa na wale wa Marsabit (asilimia 30.2), Wajir (asilimia 26.8), Samburu (asilimia 24.2), Mandera (asilimia 23.8) na Garissa (asilimia 23.7).

“Bila kujali hali zao za kazi, wanawake hutumia muda mwingi kwenye kazi zisizo na malipo kuliko wanaume. Kitaifa, watu ambao hawafanyi kazi hutumia muda mwingi kwenye shughuli zilizotajwa (asilimia 16.4) ikilinganishwa na wale wanaofanya kazi (asilimia 10.5) kila siku. Wanawake wanaofanya kazi hutumia wastani wa saa nne kwa siku katika kazi isiyolipwa, ilhali wanaume wanaofanya kazi hutumia takriban saa moja,” utafiti ulibaini.

  • Tags

You can share this post!

Taharuki punda zaidi ya 30 wakichinjwa Kitui na nyama...

Mhasibu wa KeRRa kujua hatima ya akaunti ya mahari Novemba 9

T L