• Nairobi
  • Last Updated May 16th, 2024 8:50 PM
Lopha Travellers yamulikwa abiria aliyerushwa nje basi likiwa mwendo wa kasi akifariki

Lopha Travellers yamulikwa abiria aliyerushwa nje basi likiwa mwendo wa kasi akifariki

NA SAMMY WAWERU

WAKENYA wamemshinikiza Waziri wa Uchukuzi, Kipchumba Murkomen kuchukulia hatua kali kampuni ya Lopha Travellers Sacco kufuatia kifo cha abiria aliyerushwa nje ya basi la kampuni hiyo eneo la Ruiru.

Inasemekana gari hilo lilikuwa kwa mwendo wa kasi wakati wa tukio.

Ripoti ya kuaga dunia kwa abiria huyo anayetambulika kama Nahashon, ilifichuka mapema Alhamisi.

Duru zinazohoji alifariki Jumatano wakati akiendelea kupokea matibabu, kutokana na majeraha mabaya aliyouguza.

Kituo cha afya alichokuwa akihudumiwa hata hivyo hakijabainika.

“Nahashon, jamaa aliyetupwa nje ya basi la Lopha Travellers katika eneo la Ruiru, likiwa kwenye mwendo wa kasi amefariki. Wahudumu wa matatu hiyo wanaendelea kufanya kazi kama kawaida,” Fuata Nyuki-Wa Kungu, mwanamitandao akachapisha katika ukurasa wake wa Facebook.

Inadaiwa abiria huyo alirushwa nje baada ya ugomvi kati yake na kondakta kuibuka, ikisemekana kwamba hakuwa na nauli ya kutosha.

Hukumu ya kifo 2017 kwa dereva na kondakta  

Dereva na makanga wa basi hilo kufikia sasa hawajakamatwa, Wakenya wakielekeza ghadhabu mitandaoni wakitaka wachukuliwe hatua kali kisheria.

Nambari za usajili za matatu hiyo kufikia sasa hazijatambulika.

Julai 2017, dereva wa basi linalohudumu Nairobi, kondakta na mhudumu wa kituo cha petroli eneo la Githurai 44 walihukumiwa na mahakama kifungo cha maisha kwa kudhulumu kijinsia abiria mwanamke 2014.

Akitoa hukumu ya kifo kwa Edward Gitau, Nicholas Mwangi na Meshak Mwangi, Hakimu Mkuu Francis Andayi alitaja tukio hilo kama la kinyama.

Alisema korti ilishawishika na ushahidi uliowasilishwa na afisi ya Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka ya Umma hivyo basi kuwapata na hatia washtakiwa.

Walinakiliwa kupitia video wakitekeleza ukatili huo, ikaenezwa mitandaoni na hatimaye hatua kisheria kuchukuliwa.

  • Tags

You can share this post!

MCA atoa msaada wa chakula, malazi kwa familia 500 ambazo...

Mbunge Alice Ng’ang’a alivyopendeza kwa kuvaa...

T L