• Nairobi
  • Last Updated May 9th, 2024 8:50 AM
Wakenya 36 kuwakilisha taifa Riadha za Dunia za Viziwi nchini Poland

Wakenya 36 kuwakilisha taifa Riadha za Dunia za Viziwi nchini Poland

Na VICTOR OTIENO

TAFSIRI: GEOFFREY ANENE

KENYA itawakilishwa vilivyo kwenye makala ya nne ya Riadha za Dunia za Viziwi nchini Poland mnamo Agosti 23-28 baada ya watimkaji 36 kufuzu ugani Nyayo hapo Jumanne.  

Katika mashindano ya kuchagua timu ya Kenya yaliyofanyika Juni 21-22, Simon Menza aliibuka kipenzi cha wengi aliponyakua tiketi za mbio za mita 100, mita 200 na mita 400.Katika mbio za mita 100, Menza, 23, ambaye yuko katika kidato cha kwanza katika Shule ya Upili ya Viziwi ya Pwani mjini Kilifi, alikamilisha wa kwanza kwa sekunde 11.2.

Alifuatiwa kwa karibu na David Wamira (Siaya) na Walter Malenje (Bungoma) walioandikisha 11.5 na 11.7, mtawalia.Menza alionyesha wapinzani kivumbi katika mbio za mita 200 alipovuka laini ya kumalizia mbio kwa sekunde 23.3. David Wamira (Siaya) na Charles Muthama (Machakos) walichukua nafasi mbili zilizofuata kwa sekunde 23.7 na 24.0, mtawalia.

Menza alifunga siku kwa kushinda mbio za mita 400 kwa sekunde 50.9 dhidi ya wapinzani wake wa karibu Isaac Atima (Kisii) na George Waweru (Nyeri) waliotimka 51.3 na 51.6, mtawalia. “Nafurahi sana kufuzu kuwakilisha Kenya katika vitengo vitatu kwa sababu hata sikuwa na uhakika nitahudhuria mashindano haya kutokana na ukosefu wa nauli.

Nashukuru familia yangu na walimu walioshirikiana na kunichangia nauli. Matokeo haya yamenipa motisha kwa hivyo nitaendelea kutia bidii mazoezini ili niweze kufanya vyema nchini Poland,” alisema Menza.

Katibu wa Shirikisho la Riadha za Viziwi Kenya (DAAK) Bernard Banja alisema kuwa sasa wanasubiri mwelekeo kutoka kwa serikali kuhusu kuingia kambini baada ya kukamilisha kuchagua timu. Alionya wanariadha hao dhidi ya kulaza damu akisema kuwa watatupwa nje ya kikosi wasiporidhisha mazoezini.

Kikosi cha Kenya cha wakimbiaji viziwi waliofuzu kushiriki Riadha za Dunia nchini Poland:

Mita 100 (Wanaume) – Simon Menza (Kilifi) sekunde 11.2, David Wamira (Siaya) 11.5, Walter Malenje (Bungoma) 11.7; Mita 100 (Wanawake) – Beryl Wamira (Siaya) 12.7, Rael Wamira (Siaya) 13.4; Mita 200 (Wanaume) – Simon Menza (Kilifi) sekunde 23.3, David Wamira (Siaya) 23.7;

Mita 400 (Wanaume) – Simon Menza (Kilifi) 50.9, Isaac Atima (Kisii) 51.3, George Waweru (Nyeri) 51.6; Mita 5,000 (wanaume) – Simon Kibai (Uasin Gishu) dakika 14:49, David Kipkoge (Marakwet) 15:05, Martin Gache (Uasin Gishu) 15:11, Lucas Wandia (Nairobi) 15:25, Daniel Kiptum (Uasin Gishu) 15:41, Peter Toroitich (Turkana) 15:52, Geoffrey Simiyu (Uasin Gishu) 15:54;

Mita 10,000 (wanaume) – Peter Toroitich (West Pokot) 31:46, Martin Gachie (Uasin Gishu) 31:48, Daniel Kiptum (Nandi) 31:53, Amos Lagat (Uasin Gishu) 32:27, Geoffrey Simiyu (Uasin Gishu) 33:02, Geoffrey Kamia (Nairobi) 33:26;

Mita 1,500 (Wanaume) – John Koech (Nakuru) 3:59.05, Elkana Kiprop (Kitale) 4:00.1, Kokobi Omari (Baringo) 4:00.7, Brian Kiptoo (Uasin Gishu) 4:02.2, Simon Kibai (Uasin Gishu) 4:04.9, Kioko Musyoka (Machakos) 4:16.2; Mita 800 – Elkana Kiprop (Kitale) 1:57.2, Francis Rondi (Kisii) 1:58.7, John Koech (Nakuru) 1:59.0;

Mita 3,000 kuruka viunzi na maji – Omar Kokobi (Baringo) 9:36.8, Lucas Wanjiru (Kiambu) 9:40.4, Jacob Kibet (Elgeyo Marakwet) 9:46.4, Obed Sum (Uasin Gishu) 10:12.1.

  • Tags

You can share this post!

Maeneo bunge hayataongezewa kabla ya uchaguzi mkuu wa 2022,...

Mamilioni ya fedha Kenya imetumia katika Safari Rally...