• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 10:15 PM
Maisha ya watoto 2,000 hatarini nyaya za stima zikining’inia langoni la shule

Maisha ya watoto 2,000 hatarini nyaya za stima zikining’inia langoni la shule

Na SAMMY KIMATU

NAIROBI

MAISHA ya wanafunzi zaidi ya 2,000 yamo hatarini ikiwa nyaya za stima ziliounganishwa kiholela hazitakatwa shuleni mwao haraka.

Usimamizi wa Mukuru Promotion Centre (MPC) umeiomba Kampuni ya Kenya Power na polisi kuchukua hatua ya haraka kuokoa maisha ya watoto hao kabla ya maafa kuripotiwa.

Zaidi ya hayo, MPC ilisema nyaya za stima zimeunganishwa kutoka kwa mlingoti wa taa za barabrara mkabala wa barabara ya Likoni kwenye eneo la South B, Kaunti Ndogo ya Starehe.

”Wanaokabiliwa na hatari ni wanafunzi katika shule ya upili ya St Michael, Mukuru Vocational Skills Training Centre (MVSTC) na Shule ya Msingi ya St Bakhita,” taarifa ya MPC yasema.

Nyaya za stima zimepitishwa juu ya lango la Shule, ndani ya miti karibu na MVSTC, kufungiwa juu ya miti karibu na trasfoma ya Shule.Bali na hivyo, zimepitishwa katika ua wa MPC kabla ya kuingia mtaa wa mabanda wa Maasai Village.

PICHA/SAMMY KIMATU

Vilevile, kulingana na mlinzi katika kampuni moja kwenye barabara ya Likoni, wanaohusika ni kundi la wanaume wanaouzia wakazi stima katika mtaa wa Maasai Village.Zaidi ya hayo, watu hao hushirikiana na maafisa wa kampuni ya Kenya Power na wakati mwingine polisi hushirikishwa.

“Katika sakata hii, mhudumu wa Kenya Power huwaibia stima kutoka kwa laini fulani, kutoka kwa taa za barabarani na wakati mwingine kutoka kwa kampuni,” mlinzi akaambia wanahabari.

Kulingana na upekuzi wa Taifa Leo, nguvu za umeme zikifika mtaani wa Maasai, matapeli hutoza wakazi kati ya Sh400 hadi Sh1,000 kulingana na utakavyotumia stima yenyewe.

“Kwa wanaotaka stima ya nyumba, hao hulipa Sh400 au Sh500. Walio na jokovu dukani, biashara za salun, baa na karakana nao hulipa Sh1,000 kwa kila mwezi kupata huduma hiyo,” Mama mboga mmoja mtaani wa Maasai akaambia Taifa Leo.

Kwa mujibu wa afisa mmoja wa polisi ambaye haruhusiwi kupeana habari kwa waandishi wa habari, alikiri kuna maafisa wenzao huusika katika sakata hii.“Kuna maafisa fulani wa kupeana ulinzi kwa watu wanaosambaza stima mitaani ya mabanda kote kwenye eneo la Mukuru.

Ni kazi ambayo wanaohusika hupata pesa nyingi ila hakuna pesa zozote huenda kwa serikali,” Polisi huyo akadokeza.Mkuu wa tarafa ya South B, Bw Michael Aswani Were alithibitisha utapeli na uunganishaji stima Mukuru umekita mizizi kwa miaka nyingi.

“Hata hivyo serikali ina mipango ya kuwaletea wakazi stima iliyo salama na yenye bei nafuu hivi karibuni,” Bw Were akanena.Kulingana na ripoti ya wahasibu,

  • Tags

You can share this post!

Wakenya nje ya vita vya medali ya soka ya viziwi Afrika

Mwanamume apigwa na stima aking’oa mabati eneoa la...