• Nairobi
  • Last Updated April 17th, 2024 5:55 PM
Mwanamume apigwa na stima aking’oa mabati eneoa la South B

Mwanamume apigwa na stima aking’oa mabati eneoa la South B

Na SAMMY KIMATU

NAIROBI

MWANAMUME mmoja amelazwa hospitalini ya rufaa ya Kenyatta baada ya kupigwa na stima alipokuwa aking’oa mabati ya paa ya nyumba.

Kisa hiki kilitokea jana jioni katika mtaa wa mabanda wa Hazina, South B kwenye kaunti ndogo ya Starehe.Kwa mujibu wa msaidizi wa kamishena katika eneo la South B, Bw Michael Aswani, fundi huyo alikuwa miongoni mwa mafundi waliopewa kibarua cha kubomoa nyumba ya ghorofa tatu iliyojengwa barabarani.

“Walikuwa wamepewa kazi ya kubomoa nyumba iliyokuwa katika sehemu ya kujenga barabara baada ya maafisa kutoka Mamlaka ya Kujenga Barabara za Miji (KURA) kuweka alama nyumba zinazofaa kubomolewa ili kupisha nafasi ya kujenga barabara ya Hazina/Entreprise.

Mafundi wenzake hawakujua mara moja mwenzake alikuwa amepigwa na stima akiwa peke yake juu ya jengo hilo,” Bw Were akasema.Kamanda wa polisi katika kituo cha polisi cha South B, Bw Samuel Ochoki aliwasili katika eneo la mkasa mara moja akiwa na maafisa wake punde mlio wa nyaya za stima uliposikika mtaani ndiposa wakamwokoa fundi na kumpeleka hospitalini.

Akithibitisha kisa hicho, Mkuu wa polisi eneo la Makadara, Bw Timon Odingo alisema jengo lenyewe lilikuwa hatari kwa usalama kwani lilijengwa chini ya nyaya za stima yenye uwezo wa kutoa nguvu za umeme za 33kv.

“Fundi huyo, aliinua mabati iliyokaribiana na nyaya kabla ya kupigwa na stima na kuanguka chini. Alikuwa na majeraha mgongoni na mikononi wakati alipochukuliwa akiwa ameanguka sakafuni katika ghorofa ya pili ya nyumba hiyo.

Alikimbizwa katika zahanati moja na baada ya kupatiwa huduma ya kwanza, akapelekwa katika hospitali ya rufaa ya Kenyatta alikolazwa,”Bw Odingo akanena.“Tulimtafuta mwenzetu baada ya kumwita sana bila yeye kuitika.

Tulipofika juu katika ghorofa ya pili, tulimkuta akiwa amelala chini huku nguo yake ikiwa imechomeka mikononi na mgongoni,” Seremala mmoja katika eneo la tukio akaambia Taifa Leo.

  • Tags

You can share this post!

Maisha ya watoto 2,000 hatarini nyaya za stima...

LUGHA: ‘Maankuli’ au ‘mamkuli’ ni zao la kujifunza...