• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 3:16 PM
Mama aomba korti imnyime dhamana mwanamme aliyewapiga polisi risasi

Mama aomba korti imnyime dhamana mwanamme aliyewapiga polisi risasi

Na RICHARD MUNGUTI

MAMA yake afisa wa polisi aliyepigwa risasi aliomba mahakama isimwachilie kwa dhamana mfanyabiashara anayeshtakiwa kujaribu kuwaua maafisa wawili wa polisi na weita mwanamke.

“Mama yake Konstebo Festus Musyoka Kavuthi, Bi Jane Kateve Kavuthi, ameomba hii mahakama isimwachilie mshtakiwa hadi mtoto wake atakapoanza kuzugumza,” Mbunge wa Makueni Daniel Maanzo alimsihi hakimu mwandamizi Bi Esther Kimilu.

Bw Maanzo alieleza mahakama tangu Konstebo Festus Musyoka Kavuthi alazwe katika Nairobi Hospital bado hajazugumza licha ya kufanyiwa upasuaji kwa muda wa masaa 13.Mahakama ilielezwa kuwa madaktari wako na matumaini makubwa mhasiriwa huyo atapona.

Konst Kavuthi alipigwa risasi mnamo Julai 2 2021 katika Kilabu cha Quivers Lounge kilichoko eneo la Kasarani Nairobi.Alishambuliwa akiwa na afisa mwingine wa polisi Konstebo Lawrence Muturi na Bi Felistus Nzisa.Wote watatu walilazwa Nairobi Hospital lakini Muturi na Nzisa wakatibiwa na kuruhusiwa kwenda nyumbani.

Bw Maanzo aliungana na upande wa mashtaka unaoongozwa na Bi Everlyne Onunga kuomba mshtakiwa azuiliwe hadi Jumatano.Hakimu aliombwa na kiongozi wa mashtaka Bw D Njue aamuru mshtakiwa azuiliwe katika kituo cha polisi cha Muthaiga kuwezesha Bi Onunga na afisa anayechunguza kesi hiyo kuwasilisha afidaviti kupinga mshtakiwa akiachiliwa kwa dhamana.

Mahakama ilielezwa Bi Onunga alikuwa amesafiri na “hakupata fursa ya kutosha kuwasilisha afidaviti kueleza sababu za kupinga mshtakiwa akiachiliwa kwa dhamana.”Akitoa uamuzi Bi Kimilu alisema inabidi upande wa mashtaka upewe muda wa kutosha kuandaa tetezi za kunyimwa kwa dhamana kwa Bw Dickson Njanja Mararo.

Wakili Cliff Ombeta anayemwakilisha mshtakiwa aliomba mshtakiwa aachiliwe kwa dhamana kwa vile amezuiliwa kwa zzaidi ya siku 14.Mararo amekanusha kujaribu kuwaua Kavuthi, Muturi na Nzisa.Mama yake mshtakiwa alifika kortini kusikiza yatakayomvika mwanawe.

  • Tags

You can share this post!

Majumba ya kifahari yalivyogeuka maficho ya uhalifu utalii...

Rais wa Mali anusurika kifo katika sala za Idd al-Adha