• Nairobi
  • Last Updated May 9th, 2024 6:40 PM
Mary wa Maua asimulia ugumu kumpoteza mwandani spesheli kwa mauti

Mary wa Maua asimulia ugumu kumpoteza mwandani spesheli kwa mauti

Na MWANGI MUIRURI
MBUNGE wa Maragua Bi Mary wa Maua amelia kwamba kifo cha meneja wake wa afisi ya ubunge, Bw Kennedy Kimani aliyeaga dunia Juni 10, 2023 kilimwacha hoi na mwenye hofu kuu.

Bw Kimani alikuwa wa familia moja na Bi Wa Maua ambayo inafahamika kama ya Mutuanene, asili yao ikiwa ni Kijiji cha Kahuho kilichoko Wadi ya Kahumbu katika eneobunge la Kigumo.

Kimani alifariki kupitia ajali ya barabara iliyofanyika katika barabara kuu ya kutoka Kenol kuelekea Nyeri, mpaka wa Kaunti ya Nyeri na Kirinyaga.

Bi wa Maua alikuwa amemteua kuwa meneja katika afisi yake ya eneobunge iliyoko Mjini Maragua na alikuwa amemhudumia kwa miaka 6 mfululizo.

Bw Kimani alikuwa ameandamana na kidosho mmoja ambaye alinusurika mauti katika ajali hiyo.

Katika maziko yake, Bi wa Maua alisema hajui jinsi ya kujaza pengo ambalo mwendazake ameacha katika maisha yake ya kisiasa.

“Alikuwa meneja na rafiki wangu…Ikiwa kuna mtu alielewa kuhusu ndoto zangu na kuniunga mkono kwa dhati, muite huyu aliyelala hapa.

“Huyu ndiye nilimuamini zaidi ya wote. Hata tukipanga mazishi yake, nilikuwa nikiwazia jinsi angenisaidia kuboresha ratiba lakini nikawa nakumbuka kwa majonzi ameaga,” akasema.

Alisema kuwa “nitaomba Mungu anijalie busara kutambua mwingine atakayejaza pengo lako. Itakuwa vigumu lakini miujiza hufanyika. Safiri salama hadi tutakapoonana tena”.

Mwendazake aliaga dunia akiwa na miaka 45 na amemuacha mjane na watoto watano.

[email protected]

 

  • Tags

You can share this post!

Puuzeni DNA msipate mshtuko wa mwaka, wanaume waambiwa

Ajabu mwanamke mgonjwa akitapika panya eneo la Nakuru

T L