• Nairobi
  • Last Updated May 9th, 2024 6:40 PM
Mawaziri wakuu wa zamani Algeria waongezewa hukumu

Mawaziri wakuu wa zamani Algeria waongezewa hukumu

Na AFP

ALGIERS, Algeria

Tafsiri: CHARLES WASONGA

MAWAZIRI Wakuu wawili waliohudumu chini ya utawala wa rais wa zamani wa nchi hiyo Abdelaziz Bouteflika Jumatatu waliongezewa hukumu kwa kosa la ufisadi, vyombo vya habari vimeripoti.

Ahmed Ouyahia na Abdelmalek Sellal walihukumiwa vifungo vya miaka sita na tano, mtawalia kwa uhalifu wa kiuchumi, ubadhirifu wa pesa za umma, matumizi mabaya ya afisi na kupeana tenda kinyume cha sheria,” kulingana na ripoti za magazeti ya Ennahar, Echorouk na El Hayat.

Ouyahia alihudumu kama waziri mkuu mwa mihula miwili kati ya 1995 na 2019 huku Sellal alihudumu kuanzia 2014 na 2017 na aliongoza kampeni zote za Bouteflika.

Bouteflika alijiuzulu mnamo 2019 kutokana na shinikizo kutoka kwa wanajeshi, baada ya raia wa Algeria kufanya maandamano kwa wiki kadha kupinga mpango wake wa kuwania urais kwa muhula wa tano.

Kiongozi huyo aliyeongoza kwa udikteta alifariki mwezi huu akiwa na umri wa miaka 84 na akazikwa bila heshima na taadhima iliyopewa watangulizi wake.Baada ya kuondolewa kwake mamlakani, wapelelezi walianzisha chunguzi mbalimbali dhidi ya wafanyabiashara waliokuwa washirika wake.

Baadhi yao walikamatwa kwa kusumwa gerezani kwa tuhuma za ufisadi.

  • Tags

You can share this post!

Morogo akana kituo cha polisi cha Syokimau kilikuwa na seli

Masharti kwa makocha wa soka Kenya