• Nairobi
  • Last Updated May 20th, 2024 5:52 PM
Masharti kwa makocha wa soka Kenya

Masharti kwa makocha wa soka Kenya

NA JOHN ASIHUNDU

SHIRIKISHO la Kandanda Nchini (FKF) halitawakubalia wakufunzi wasio na vyeti vifaavyo kuandaa timu za ligi kuu pamoja na ligini nyingine za chini.

Kulingana na maagizo hayo yaliyowekwa sahihi na wakuu wa soka nchini Nick Mwendwa, Barry Otieno na Petra Doris, lazima mtu awe na cheti cha CAF C Diploma ili akubaliwe kuandaa timu ya Ligi Kuu (FKF-PL), Ligi Kuu ya Wanawake (WPL), Supa Ligi ya Taifa (NSL), Daraja la Kwanza, Ligi ya Wanawake Daraja la Kwanza na Ligi ya Daraja la Pili.

Wakufunzi kutoka mataifa ya kigeni watahitajika kuwa na cheti cha A License.Wakufunzi wa makipa wanaotaka kuandaa timu za FKF- PL, WPL, NSL na Daraja la Kwanza watatakiwa kuwa na angalau cheti cha FKF License Diploma, huku madaktari wakihitajika kutuma CV zao kwa idara ya kiufundi ya FKF ichunguzwe kabla wapate idhini ya ktekeleza kazi yao.

Makocha wanaotaka kuandaa timu za Ligi ya Wanawake Daraja la Kwanza (FKF WD 1) na FKF Daraja la Pili lazima wawe na cheti cha FKF D License Diploma.

  • Tags

You can share this post!

Mawaziri wakuu wa zamani Algeria waongezewa hukumu

Kinoti akwepa hukumu