• Nairobi
  • Last Updated May 9th, 2024 6:40 PM
Morogo akana kituo cha polisi cha Syokimau kilikuwa na seli

Morogo akana kituo cha polisi cha Syokimau kilikuwa na seli

Na RICHARD MUNGUTI

AFISA wa polisi wa Utawala Koplo Stephen Morogo anayeshtakiwa kwa mauaji ya wakili Willie Kimani Jumatatu alikana kabisa kulikuwa na seli za kuwazuilia mahabusu katika kampuni ya Syokimau.

Akijitetea katika kesi ya kuwaua Kimani , Josephat Mwenda na Joseph Muiruri Juni 23,2016 , Koplo alikana alikuwa kazini siku hiyo.Koplo Morogo alieleza Jaji Jessie Lesiit kwamba siku hiyo hakuwa kazini.

“Sikuwa kazini siku hiyo. Nilishinda kwa nyumba nimelala,” alisema Koplo Morogo.Alieleza mahakama kwamba ijapokuwa utaratibu wa kazi ulionyesha kwamba alikuwa kazini na Konstebo Sylvia Wanjiku Wanjohi, yeye alikuwa kwa nyumba akipanga mazishi ya mke wa mwanawe.

Mshtakiwa huyo alisema ushahidi wa simu unadhihirisha hakuwa kazini.Lakini mshtakiwa huyo alijipata tabaani mahakama kitabu kinachoonyesha maafisa wa polisi waliokuwa kazini kuanzia Juni 20-22,2016.

Ijapokuwa mshtakiwa huyo alieleza korti alikuwa kazini , alishindwa kueleza sababu hakujaza kitabu hicho cha Occurrence Book (OB) kuonyesha muda alioingia kazini na aliotoka.

Mshtakiwa alihojiwa vikali na wakili wa familia za wahasiriwa Fred Ojiambo na pia kiongozi wa mashtaka Bw Nicholas Mutuku.Kutokana na majibu aliyotoa mahakama ilielezwa mshtakiwa hakuwa akisema ukweli.

Pia alikana kortini hakumfahamu Inspekta Fredrick Lelimani wanayeshtakiwa pamoja kwa mauaji ya Kimani , mteja wake Mwenda na dereva wa teksi Muiruri.Watatu hao walitekwa nyara walipokuwa wanatoka mahakama ya Mavoko mnamo Juni 23, 2021 , kisha wakazuiliwa katika kampi ya Syokimau.

Ushahidi ulisema walitolewa kwenye seli na kuuawa katika eneo la Soweto kisha maiti zao zikatupwa katika mto Athi River.Mahakama ilielezwa Morogo na Wanjiku ndio waliokuwa kazini siku hiyo Kimani alipozuiliwa katika kampi hiyo.

Kesi inaendelea kusikizwa.

  • Tags

You can share this post!

Fati arejea kikosini na kuwabeba Barcelona dhidi ya Levante...

Mawaziri wakuu wa zamani Algeria waongezewa hukumu