• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 5:50 AM
Mholanzi aliyetupwa rumande kwa madai ya kuchafua watoto Uasin Gishu apewa dhamana

Mholanzi aliyetupwa rumande kwa madai ya kuchafua watoto Uasin Gishu apewa dhamana

Na RICHARD MUNGUTI

RAIA wa Uholanzi anayekabiliwa na kesi ya kuwadhulumu watoto wa umri wa miaka 16 na 17 kimapenzi katika Kaunti ya Uasin Gishu kati ya 2022 na 2023 ameachiliwa kwa dhamana.

Jan Int Veld almaarufu Dad Ok almaarufu Teacher Jan almaarufu Mzungu alipewa dhamana ya Sh2milioni na wadhamini wawili wa kiasi hicho.

Akimwachilia kwa dhamana hakimu mkazi Bi C C Oluoch anayesikiza na kuamua kesi za dhuluma dhidi ya watoto alisema upande wa mashtaka ulishindwa kuthibitisha atatoroka akiachiliwa kwa dhamana.

Bi Oluoch alisema dhamana ni haki ya kila mshtakiwa.

“Upande wa mashtaka haukuwasilisha ushahidi kuthibitisha mshtakiwa atatoroka akiachiliwa kwa dhamana,” alisema Bi Oluoch.

Hakimu huyo alisema mshtakiwa ameanzisha mashirika mawili ya kutoa ufadhili kwa jamii katika miji ya Kisumu na Eldoret.

Mzungu alikana mashtaka matano ya kuwadhulumu watoto hao wa umri wa miaka 16 na 17 kimapenzi.

Upande wa mashtaka ulipinga Mzungu akiachiliwa kwa dhamana ukisema “akiachiliwa atatoroka kwa vile adhabu ni kali ya mashtaka yanayomkabili.”

Mzungu alikuwa amezuiliwa katika  gereza la Viwandani hadi hapo jana.

Pia alirudishwa kukaa mle hadi atakapowasilisha dhamana.

Miongoni mwa mashtaka yanayomkabili ni pamoja na kuwaonyesha filamu za ngono watoto hao kwa nia ya kuwashawishi washiriki ngono naye.

Mzungu alishtakiwa siku 17 baada ya raia wa Amerika Terry Ray Krieger kushtakiwa katika mahakama ya Mavoko kwa kuwadhulumu kimapenzi watoto.

Krieger, mwenye umri wa miaka 68, aliyefungwa na mahakama ya Nairobi miaka 50 na kuachiliwa katika mazingira tata na Jaji Momanyi Bwonwong’a aliyestaafu, amezuiliwa katika gerezani la Kitengela hadi Feburuari 22, 2024 kesi itakapotengewa siku ya kusikizwa.

Bi Oluoch alitenga kesi dhidi ya Mzungu kusikizwa Januaru 9, 2024.

  • Tags

You can share this post!

Barobaro aliyemfuata shugamami kwake nyumbani atumiwa...

Serikali yawekea bodaboda kafiu eneo la South B

T L