• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 8:46 PM
Mkenya aliyechapwa viboko na Mchina kulipwa Sh3 milioni

Mkenya aliyechapwa viboko na Mchina kulipwa Sh3 milioni

Na SAM KIPLAGAT

MKENYA ambaye alinaswa kwenye video akichapwa na waajiri wake raia wa China mwaka uliopita, amelipwa fidia ya Sh3.07 milioni kwa kutimuliwa kazini kinyume cha sheria.

Jaji wa Mahakama ya Ajira, Mathews Nderi aliagiza kwamba, usimamizi wa hoteli ya Wachina iliyo katika mtaa wa Kileleshwa, walipe fidia hiyo mwanaume aliyetambuliwa kama SOS.

Mahakama ilisema mwanaume huyo aliyefanya kazi hotelini humo kwa miezi mitatu, pia alidhulumiwa kingono.

Alidhulumiwa na raia hao wa kigeni baada ya kukataa kushiriki ngono na mwajiri wake ambaye alinaswa kwa camera ya simu akimchapa viboko.

Serikali ilimrejesha kwao raia huyo wa China kabla ya kufikishwa kortini kujibu mashtaka.Mahakama ilisema mlalamishi alidhalilishwa na kupatwa na msongo wa mawazo baada ya kuchapwa viboko na mshtakiwa.

Mlalamishi, kupitia kwa wakili wake Steve Mogaka, pia alimshtaki waziri wa Usalama Fred Matiang’i na Mkuu wa Sheria lakini korti ikasema hakukuwa na ushahidi wa kuonyesha kwamba waliruhusu unyama huo.

Mahakama iliagiza alipwe fidia ya Sh3 milioni kwa kukiuka haki zake za kibinadamu na Sh72,000 kwa kumtimua bila kufuata sheria.

 

You can share this post!

Kalonzo, Kivutha waahidi kushirikiana katika maendeleo

Kocha Vieira kurejea Arsenal kuwinda vipaji vya kuboresha...