• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 11:35 AM
Mlanguzi sugu wa dawa za kulevya aliyelemea askari

Mlanguzi sugu wa dawa za kulevya aliyelemea askari

NA TITUS OMINDE

MFANYIBIASHARA mmoja mjini Eldoret anayekabiliwa na kesi ya ulanguzi wa dawa za kulevya, amekamatwa tena kwa kupatikana heroini.

Chrispine Omondi alitiwa nguvuni na polisi wa kupambana na mihadarati kwa madai ya kuwa na gramu 54 za heroini.

Wiki iliyopita, Omondi, 38, alishtakiwa kwa kupatikana na kilo 4.5 za bangi kinyume cha sheria.

Mwendesha mashtaka aliambia mahakama Alhamisi katika mahakama Eldoret kuwa mshukiwa alikamatwa na maafisa wa upelelezi katika eneo la Roadblock kiungani mwa mji wa Eldoret.

Korti ilielezwa kwamba mnamo Mei 15, 2023 katika eneo la Roadblock, Kaunti Ndogo ya Turbo, mshtakiwa alikamatwa akiwa na dawa ya kulevya zinazoshukiwa kuwa heroini ya uzani wa gramu 54.

Mshtakiwa hata hivyo alikana shtaka linalomkabili.

Afisa wa upelelezi aliambia mahakama kwamba thamani ya dutu (substance) hiyo bado haijajulikana.

Wakili wa serikali Jairus Onkoba aliomba mahakama kuruhusu polisi kupeleka dawa hiyo kwa wanakemia wa serikali ili kubaini ikiwa ni heroini na pia kuthibitisha thamani yake ya mtaani.

Ombi la mshtakiwa kuachiliwa kwa bondi kupitia wakili wake John Ombego lilikataliwa na mahakama, kutokana na rekodi mbaya ya mshtakiwa.

“Mshtakiwa ametambuliwa kuwa mlanguzi wa dawa za kulevya. Alikuwa katika mahakama iyo hiyo siku chache zilizopita na aliachiliwa kwa dhamana kwa karibu mashtaka sawa. Hafai kuachiliwa kwa dhamana,” Bw Onkoba aliambia mahakama.

Wakili wake Bw Ombego alipinga ombi hilo akidai kuwa sababu zilizotolewa na upande wa mashtaka kukataa bondi ya mteja wake haziko ndani ya sheria.

Mahakama itatoa uamuzi kuhusu kuachiliwa kwake kwa dhamana baadaye leo, Alhamisi Mei 19.

Wiki moja iliyopita Omondi aliachiliwa kwa dhamana ya Sh300, 000 baada ya kukana kuwa na dawa za kulevya kinyume na kifungu cha tatu cha sheria ya kudhibiti dawa za kulevya ya mwaka 1994.

Alishtakiwa kuwa mnamo Mei 5 katika eneo la Roadblock- Barabarani na Kaunti Ndogo ya Turbo alipatikana na kilo 4.5 za bangi ya thamani ya sh90, 000.

  • Tags

You can share this post!

Wabunge Babu Owino na Peter Salasya walimana mitandaoni

Mashambulio makali nchini Sudan mahitaji ya chakula...

T L