• Nairobi
  • Last Updated May 13th, 2024 9:17 PM
Serikali yashirikiana na FAO kuibuka na mpango maalum kukabili wadudu waharibifu wa mimea

Serikali yashirikiana na FAO kuibuka na mpango maalum kukabili wadudu waharibifu wa mimea

Na SAMMY WAWERU

SERIKALI kwa ushirikiano na Shirika la Chakula na Kilimo (FAO-UN) imeibuka na mpango wa kudumu kukabili wadudu waharibifu kwa mimea.

Katibu katika Wizara ya Kilimo, Mifugo na Samaki Prof Boga Hamadi, amesema mpango huo pia unajumuisha kukabili nzige na viwavijeshi.

Mikakati hiyo imejiri baada ya Kenya kufanikiwa kukabili kikamilifu nzige na viwavijeshi.

“Tumekuwa na kero ya viwavijeshi na nzige hatujui litakalojiri baadaye, hivyo basi tunahitaji kuwa tayari kila wakati,” akasema Prof Boga.

Mwaka wa 2019 na 2020, Kenya ilikumbwa na mkurupuko wa nzige waharibifu, hasa katika maeneo kame.

Aidha, zaidi ya kaunti 32 ziliathirika na mikumbo hiyo miwili.

Akizungumza Kilimo House, jijini Nairobi, katibu huyo wa kitengo cha mimea alisema wadudu hao walikabiliwa chini ya athari haba kwa mimea, malisho ya mifugo na kwa mazingira.

Mbali na FAO, serikali pia ilishirikiana na Benki Kuu ya Dunia kuangamiza wadudu hao hatari.

Prof Boga alitoa tangazo la mpango huo wakati akipokea lori lilitolewa kama msaada na FAO kwa Wizara ya Kilimo ili kusaidia kusafirisha pembejeo na dawa za kukabili wadudu.

“Limeboreshwa ili kusafarisha dawa hatari za wadudu na pembejeo nyinginezo. Ni hatua kubwa tumepiga mbele, na inaashiria uhusiano na ushirikiano wetu wa karibu na serikali ya Kenya,” akasema Bi Carla Mucavi, Mwakilishi wa FAO hapa Kenya.

  • Tags

You can share this post!

West Ham ya Moyes yazidisha masaibu ya Spurs ligini

Maswali Ruto akifokea Museveni

T L