• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 8:50 AM
Mshukiwa wa wizi alivyohangaisha kikosi cha DCI kichakani kwa saa sita

Mshukiwa wa wizi alivyohangaisha kikosi cha DCI kichakani kwa saa sita

Na MWANGI MUIRURI 

Afisa wa kitengo cha GSU aliyetambuliwa kama Isaac Wanzala na anayeshukiwa kunyemelea kambi na kuiba bunduki mbili na risasi 20 ametiwa mbaroni katika Kaunti ya Busia.

Gumzo mtaani ni kwamba ni kama Wanzala aliwahurumia maafisa hao na akajisalimisha kuwaepushia balaa ya kurudi stesheni bila kumpata na pia silaha hizo.

Taarifa kutoka kwa kitengo cha Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Bw Amin Mohammed ya Septemba 3, 2023 ilisema kwamba Wanzala alitekeleza wizi huo mnamo Agosti 23, 2023.

Alidaiwa kwamba akiwa katika makataa ya kutoonekana kazini kwa msingi wa kusimamishwa kazi kutokana na utukutu, aliingia kambini kama mwizi.

Alisemekana kuingia katika Kambi ya Korngotuny wakati wa usiku na bila kujulikana, akatoka akibeba bastola mbili na risasi 20.

Alidaiwa kwamba alisafiri nazo hadi kijijini mwao Mabonge kilichoko eneo bunge la Nambale katika Kaunti ya Busia na akazificha karibu na mto shambani mwa babake.

Bila kuelezea jinsi iligunduliwa baadaye kwamba Bw Wanzala ndiye alikuwa mwizi kambini, Bw Mohammed alisema kwamba maafisa wa DCI waliokuwa wamejihami hata na vitoa machozi na bunduki kalikali walitumwa kumsaka.

“Baada ya uchunguzi wa kina na kujipiga msasa, tuligundua kwamba Bw Wanzala ndiye alikuwa mwizi na tukamtumania atiwe mbaroni,” taarifa ikasema.

Bw Wanzala naye alionekana kutambua anasakwa kwa sababu DCI walipofika kwao bomani, alikuwa kwa shamba la miwa akijificha.

Anasemekana kwamba kumtoa kwa hiyo miwa kulidumu masaa kadha na operesheni iliyozinduliwa saa 10 usiku iliisha saa nne asubuhi.

Ni wakati maafisa hao wa DCI walianza kuonyesha nia ya kumuua ambapo alijisalimisha, taarifa hiyo yasema.

Baada ya kujisalimisha, alielekeza maafisa hao hadi kwa kingo za mto Sio ambapo aliwaonyesha alikokuwa amezika silaha hizo.

Ndipo akakamatwa na silaha zikatwaliwa na kwa sasa, anangojea kuwasilishwa mahakamani.

  • Tags

You can share this post!

Warembo 26 kutoka Ethiopia wanaswa wakiwa...

Benki ya AfDB yaahidi kutoa Sh3.6bn kusaidia kukabiliana na...

T L