• Nairobi
  • Last Updated May 9th, 2024 6:40 PM
Muturi aelekeze Mlima Kenya waseme kwa sauti moja

Muturi aelekeze Mlima Kenya waseme kwa sauti moja

Na KINYUA BIN KING’ORI

Tangu spika wa Bunge la kitaifa Justin Muturi kutawazwa kuwa msemaji wa Jamii ya Mlima Kenya katika ulingo wa kisiasa, kumetokea mgawanyiko na malumbano makali huku viongozi wakiendelea kukwaruzana kila uchao.

Kumeibuka makundi matatu; moja likiunga mkono mtoto huyo wa mbeere kaunti ya Embu katika eneo la mlima Kenya mashariki, linaongozwa na Gavana wa Meru, Kiraitu Murungi huku kundi la lingine likikosoa kutawazwa kwake, viongozi wanaopinga ujio wake wanajumuisha magavana Mwangi wa Iria (Murang’a), Nderitu Murithi (Laikipia), Francis kimemia (nyandarua) aliyekuwa gavana wa kwanza wa Kiambu, William kabogo miongoni mwa wengine huku kundi la wasomi likiwa halijatangaza kumuunga mkono au kupinga.

Kundi la pili , linamchukulia Bw Muturi kama kiongozi limbukeni kisiasa ambaye hana ujasiri wa kutetea maslahi ya jamii ya eneo la Kati kisiasa Wala kuwa na umahiri wa kuwaunganisha viongozi kuchukua Msimamo mmoja Kwa manufaa ya jamii hiyo kisiasa 2022.

Wanasisitiza spika huyo hawezi kuhakikisha Jamii hiyo imefaulu kuwa na mgombezi wa urais 2022 ikizingatiwa kura nyingi kutoka eneo hilo. Wanaomba mikakati Zaidi kusukwa kuipa Jamii hiyo matumaini katika uchaguzi wa 2022.

Tayari, wanasiasa maarufu wamepuuzulia mbali kutawazwa kwa kiongozi huyo, na ikiwa kweli mbunge huyo wa zamani wa siakago anayo nia ya kufanikiwa Katika azma yake ya kuwa msemaji wa Jamii ya mlima Kenya hana budi kuibuka na mbinu mpya kuvutia imani na kupata ungwaji mkono kutoka Kwa viongozi na wananchi Kwa jumla kutoka eneo la Kati bila kujali ikiwa ni mkikuyu, meru, Muembu au mutharaka.

Mwanasiasa huyo anahitaji weledi na ustadi mkubwa kuonekana kama kiongozi mwenye utaalamu, mkomavu, mnyenyekevu, asiye na kiburi, msikivu bila kusahau wajibu wa kupalilia umoja na amani katika Jamii ya mlima Kenya na Kenya Kwa jumla.

Lakini inasikitisha kutambua tayari, Muturi amefeli mtihani huo, Kwa kujitokeza hadharani kuzua malumbano na viongozi wanaopinga kutawazwa kwake ni ishara tosha hawi kiongozi ambaye anaweza kuimarisha umoja katika eneo hilo.Matamshi yake kukejeli mahasimu wake kisiasa majuzi akiwa katika la St peter’s Kaunjira National independent church of Africa (NICA) kaunti ya meru, aliwasuta Kwa kisingizio cha wazee waliomtawaza kukosewa heshima.

Aliwataja kama viongozi wanaokosea pia utamaduni heshima na kukiuka haki ya kidemkrasia ya wazee hao Kwa mujibu wa katiba.Alijipiga kidari Kwa kuwaambia viongozi hao kuwa na nidhamu na kuheshiimu maoni ya wenzao.

Matamshi hayo ndiyo yanamwonyesha spika huyo kama kiongozi asiyekumbatia kukosolewa ambaye anawachukulia wale wanaopinga azma yake kama maadui na watu wasio na nidhamu Kwa wazee na utamaduni Kwa jumla. Ikiwa ndiyo mbinu yake ya uongozi hawezi kuwa msemaji wa Jamii ya mlima Kenya kisiasa, kiuchumi Wala kijamiiBw Muturi anafaa kumeza ukweli mchungu kwamba baadhi ya viongozi wanaompinga wakiwemo magavana ni watu wenye ushawishi mkubwa mashinani na hata serikalini.

Umaarufu wa wengi wao kisiasa hauwezi kulinganishwa na wake, hivyo kutawazwa na baadhi ya wazee kuwa msemaji wa Gema haiwi sababu yake kujiona bora na mwenye ushawishi, la hasha! Anafaa awe mstari wa mbele kuhakikisha jamii hiyo inazungumza kwa sauti moja kisiasa 2022.

Hilo kutimia sharti, athibitishe yeye si kibaraka chake Rais uhuru Kenyatta ambaye anebakisha miezi 13 kustaafu. Ikiwa kweli kutawazwa kwake kumeungwa mkono na Rais itakuwa mchongoma kushawishi wananchi wa kawaida Wa eneo la mlima Kenya kumuunga mkono Kwa imani ya uaminifu 2022 ikiwa atatangaza kuwania wadhifa wa urais 2022.

Anafaa kutambua wakenya hawapendelei kuchaguliwa kiongozi na watu fulani Kwa maslahi yao kisiasa, bali ni matumaini yao kujichagulia viongozi wapendao wao wenyewe akiwemo Rais bila kulazimishwa.

Mbinu bora kwake Kwa Sasa anahitaji kuunda mikakati ya mapema kujipigia debe kama mmoja wa vigogo watakaowania urais 2022, bila kuchelewa awe na moyo wa hariri kuleta maridhiano na utangamano Kwa kuwafikia walinzani wake kuhakikisha anaungwa mkono na asilimia kubwa ya watu wa maeneo ya kati.

Japo wengi wa vigogo wa kisiasa wanamchukulia Bw Muturi kwa njia ya kimzaha, dharau na urahisi wa aina yake akizingatia siasa za umoja na unyenyekevu ataibuka mwaniaji anayetikisa vigogo wa zamani katika uchaguzi wa 2022 japo atashindwa Vibaya na Naibu Rais Dkt William Ruto au kinara wa upinzani Raila odinga ikiwa watawania urais pia

  • Tags

You can share this post!

‘Ushirika wa ODM, Jubilee moto wa kuotea mbali’

Kesi ya Echesa kusikizwa faraghani