• Nairobi
  • Last Updated May 9th, 2024 8:50 AM
Kesi ya Echesa kusikizwa faraghani

Kesi ya Echesa kusikizwa faraghani

Na RICHARD MUNGUTI

KESI ya kashfa ya ununuzi wa vifaa vya kijeshi vya gharama ya Sh39.5bilioni dhidi ya aliyekuwa Waziri wa Michezo Rashid Echesa, jana ilisikizwa faraghani kufuatia ombi la Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) Bw Noordin Haji.

Hakimu mwandamizi Bw Kennedy Cheruiyot aliwaagiza wanahabari na umma utoke kortini kabla ya maafisa wakuu wa kijeshi kuanza kutoa ushahidi.Akiruhusu ombi la DPP ushahidi wa maafisa watatu wakuu wa kijeshi upokelewe faraghani, hakimu alisema ombi hilo liko na mashiko kisheria.

“Kesi hii iko na umuhimu mkubwa kwa umma lakini itabidi ushahidi wa maafisa wakuu wa kijeshi wasikizwe faraghani. Ushahidi wao unaguzia masuala ya usalama wa nchi,” alisema Bw Cheruiyot.

Mahakama ilielezwa na kiongozi wa mashtaka Bw Kennedy Panyako kwamba suala la usalama ni nyeti na mahakama yapasa kuichukuliwa kwa uzito.Mawakili Evans Ondieki, Dancan Okatchi na wengine watat hawakupinga kesi hiyo ikisikizwa faraghani.

Akitoa uamuzi hakimu aliruhusu kesi hiyo isikizwe faraghani ili masuala nyeti ya usalama yasianikwe hadharani.Bw Echesa ameshtakiwa pamoja na Daniel Otieno Omondi almaarufu Jenerali Juma, Clifford Okoth Onyango almaarufu Paul, Kennedy Oyoo Mboya, Chrispin Oduor Odipo na Pzels Company Limited.

Wamekana mnamo kati ya Oktoba 2, 2019 na Februari 13, 2020 walikula njama za kumlaghai Bw Kozlowski Stanley Bruno Sh11,500,000 wakidai watampa kandarasi ya kununulia idara ya majeshi vifaa mbali mbali.

  • Tags

You can share this post!

Muturi aelekeze Mlima Kenya waseme kwa sauti moja

Watoto wapewe basari bila ubaguzi – Magoha