• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 8:55 PM
Muuzaji wa dhahabu feki apatikana mashtaka ya kujibu

Muuzaji wa dhahabu feki apatikana mashtaka ya kujibu

Na RICHARD MUNGUTI

HAKIMU mkuu wa Nairobi Francis Andayi Ijumaa alimpata na kesi ya kujibu mfanyabiashara Bw Kevin Obia alimaarufu Kevin Kleigh anayekabiliwa na shtaka la kupokea Sh13.7m kwa njia ya undanganyifu mnamo Mei 1 2015.

Bw Obia alikana kumfuja raia wa Austria Bw Christian Gallati akijifanya alikuwa na kilo saba za dhahabu ambazo angelimwuzia.

Pia ameshtakiwa kwa kujaribu kumtapeli Bw Gallati Dola za Marekani ($) 570,000 (Sh54m) mnamo Mei 18 2015 akijifanya alikuwa na kilo 13 za dhahabu ambazo angelimwulizia.

Akijitetea, Bw Obia anayeshtakiwa kupokea Euro 127,000 sawa na Sh13.7milioni kutoka kwa raia wa Australia Bw Christian Gallati akimdanganya atamuuzia kilo saba za dhahabu alieleza korti “hajui chochote kuhusu biashara ya dhahabu.”

Huku akimsihi Bw Andayi amwachilie , Bw Obia, alisema “polisi walimwelekea alipokea Sh13.7m na kujaribu kumfuja Bw Gallati dolla za marekani 570,000 (Sh54.1milioni) katika biashara feki ya dhahabu.”

“Mimi sijui chochote kuhusu biashara ya dhahabu. Mimi nahusika na masuala ya burundani na wala sio dhahabu,” Bw Obia alimweleza hakimu.

Bw Andayi alimsukuma Bw Obia kizimbani kujitetea baada ya upande wa mashtaka unaongozwa na Bi Angela Fuchaka kukamilisha kutoa ushahidi dhidi ya mshtakiwa.

“Uko na kesi ya kujibu,” Bw Andayi alimweleza Bw Obia.

Samuel Muturi, dereva wa Obia atoa ushahidi katika kesi ya bosi wake..Picha/RICHARD MUNGUTI

Hakimu alisema baada ya kuchambua ushahidi wote uliowasilishwa na Bi Fuchaka , mshtakiwa yuko na kesi ya kujibu.

Bw Obia alitoa ushahidi akiwa upande wa mashtaka na kuulizwa maswali na Bi Fuchaka.

Akijijaribu kujianusua na kesi hiyo, Bw Obia alisema alikutana na wageni wake katika hoteli ya Hilton Nairobi kujadili biashara ya burundani.

“Baada ya kufanya mkutano na wageni wangu katika hoteli ya Hilton maafisa watatu wa polisi walinikamata na kunipeleka kituo cha polisi cha Central ambapo walinifungulia mashtaka,” alisema Bw Obia akijitetea.

Dereva wake Bw Samuel Ndung’u Muturi alieleza mahakama mnamo Mei 18 2015 alimpeleka Bw Obia katika hoteli ya Hilton kukutana na wageni wake.

“Tuliingia pamoja hotelini. Nilikunywa chai. Wageni wake waliingia makundi mawili. Kundi la kwanza halikukawia. Kundi la pili lilifika kisha likatoka naye nje ya hoteli,” alisema Bw Muturi.

Bw Muturi aliongeza , “ Baada ya dakika kama nane Bw Obia alinipigia simu na kunieleza nipeleke gari nyumbani kwake na kuiacha pale.”

Dereva huyo alisema hakuona wageni waliofika kwanza wakimpa mshtakiwa chochote.

“Je ulikuwa kazini Mei 1 2015?,” Bi Fuchaka alimwuliza Bw Muturi. “Hapana sikuwa kazini. Siku hiyo ilikuwa Leba Dei na nilikuwa nyumbani napumzika,” alijibu Bw Muturi.

“Kwa hivyo kama Bw Obia alifanya kitu huwezi kujua,” Bi Fuchaka alimwuliza tena.

Akijibu Bw Muturi alisema “hajui ikiwa mwajiri wake alipokea pesa Mei 1 2015 ama hakupokea kwa vile hawakuwa pamoja siku hiyo.”

Bw Obia aliye nje kwa dhamana anabakiliwa na shtaka la kumlaghai Bw Galatti Euro 127,000 (SH13.7m) mnamo Mei 1 2015 katika hoteli ya Hilton.

Kesi itaendelea Machi 1, 2021.

You can share this post!

Mchuano wa mkondo wa pili wa Europa League kati ya Arsenal...

Jinsi madiwani wanavyotishwa kupitisha BBI