• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 8:55 PM
Mwanafunzi wa chuo akana kumiliki nakala za KCPE na KCSE kinyume cha sheria

Mwanafunzi wa chuo akana kumiliki nakala za KCPE na KCSE kinyume cha sheria

NA RICHARD MUNGUTI

MWANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha Zetech alishtakiwa Jumatatu kwa kupatikana na karatasi za mtihani wa kitaifa unaoendelea wa shule za upili Kidato cha Nne (KCSE).

Oscar Brighton almaarufu Jagongo pia alishtakiwa kwa kupatikana na mtihani wa Darasa la Nane KCPE uliokamilika Machi 9, 2022.

Kiongozi wa mashtaka Bw Anderson Gikunda alimweleza hakimu mkuu Wendy Kagendo kwamba mshtakiwa alikutwa na polisi akiwa ameweka mitihani hiyo katika simu yake.

Mashtaka mawili dhidi ya mshtakiwa yalisema kati ya Machi 7 na 10 mwaka huu 2022 alihifadhi katika simu yake karatasi za mtihani wa KCPE na KCSE.

Mshtakiwa pia alikabiliwa na shtaka la kutuma nakala za mtihani kwa mtu mwingine.

Mshtakiwa aliomba aachiliwe kwa dhamana akisema “hatatoroka bali atahudhuria vikao vyote vya mahakama.”

Mahakama ilimwachilia mshtakiwa kwa dhamana ya Sh1,000,000 hadi Aprili 1, 2022 kesi itakapoanza kusikizwa.

Akishindwa kutoa dhamana hiyo hakimu aliamuru mshtakiwa alipe dhamana ya pesa taslimu Sh500,000.

Bi Kagendo pia aliamuru Bi Gikunda amkabidhi mshtakiwa nakala zote za ushahidi.

  • Tags

You can share this post!

Wakazi 200 wajitokeza kwa upanzi wa miti kuhifadhi vyanzo...

Maumau wawasilisha kesi kortini wakitaka Ruto atimuliwe...

T L