• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 10:50 AM
Mwanamke aponea kifo risasi ya polisi ilipomkosa

Mwanamke aponea kifo risasi ya polisi ilipomkosa

Na SAMMY KIMATU

MWANAMKE mmoja aliponea kifo kwa tundu la sindano baada ya jaribio la kupigwa risasi na ofisa aliyedaiwa kuwa ni polisi kumkosa katika baa moja mtaani wa mabanda wa Mukuru-Hazina, South B.

Kwa mujibu wa walioshuhudia kisa hicho mwendo wa saa kumi na mbili jioni, mwanamume aliyevalia sare za polisi aliwasili mtaani na kupanda orofa ya mabati kulioko na baa.

“Mwanamume huyo alichomoa bastola yake na kuitayarisha kufyatua akirelekea kilabuni. Ghafla tulisikia mlio wa risasi kutoka kilabuni kila mtu akitorokea usalama wake,” Mwenyekiti wa usalama kataika mtaa wa Mukuru-Hazina, Bw David Kiarie akasema.

Sukunde chache zikifofuata, mwanamke alichomoka kutoka kilabuni bila viatu akifuatwa mbio na vijana watatu walioaminika walikuwa wateja waje katika baa ambayo haijaandikwa jina.

Mkuu wa polisi eneo la Makadara, Bw Timon Odingo aliambia Taifa Leo amethibitisha kisa hicho na kuongeza kwamba kinachunguzwa na maafisa wa kitengo cha Jinai.

“Kulingana na ripoti tuliyo nayo, maafisa wa polisi wa kitengo cha jinai wanachunguza kisa hiki kililichosababisha hofu mitaani mitatu iliyopakana na eneo la kituo. Bali ni kisanga tunachokichukulia kama cha kindani kwa upande wa polisi,” Bw Odingo akanena.

Kulingana na taarifa ambayo Taifa Leo ilipata kivyake, jina na ofisa huyo ni Bw Geoffrey Thuo, 59 anayehudumu kituoni vha polisi cha Jogoo naye mwanamke akitambuliwa kwa jina Bi Zaweria Wangari, 28.

Uchunguzi wetu ulibaini kwamba Bi Wangari alitofautiana na Bw Thuo baada ya uhusiano wao wa kimapenzi kuingia ndoa.

“Mwanamke, Bi Wangari alikiri walikuwa na uhusianio wa kimapenzi na Bw Thuo ila Bi Wangari aliamua kuachana na Bw Thuo akisema hataki kuitilafiana na ndoa yake na mkewe wa ndoa. Hata hivyo, Bw Thuo alimtishia maisha Bi Wangari na kumhahidi atakuja kumwua siku moja,” mdokezi wetu akatamka.

Bw Thuo ndiye mmiliki wa kilabu huku Bi Wangari akiwa mfanyakazi katika baa lenyewe.

Walioshuhudia kisa kiki walisema Bw Thuo sawia na Bi Wangari walikuwa na vumbi nguoni zao upande wa mgongo ishara kwamba walikabiliana sakafuni ndani ya kilabu kabla ya kupata nafasi ya kuhepa.

Hofu ilitanda hapa mtaani Mukuru-Hazina na mitaa ya mabanda ya Mukuru-Maasai na Mukuru-Kaiyaba,” mama mmoja aliye na biashara ya kuuza chakula katika eneo la kisa akanena.

Kuna ongezeko la visa vya polisi kuhusika na visanga vinavyotokana na mapenzi huku polisi wakituhumiwa kwa kutumia silaha zao dhidi ya raia vimbaya na kinyume cha sheria.

  • Tags

You can share this post!

Mbinu mpya zinazotumiwa kudumisha usalama mitaani

Watoto wanne waliotekwa nyara Thika wapatikana

T L