• Nairobi
  • Last Updated May 8th, 2024 8:55 PM
Mwanamume aliyenyimwa kitambulisho kulipwa fidia

Mwanamume aliyenyimwa kitambulisho kulipwa fidia

Na BRIAN OCHARO

SERIKALI imeagizwa kumlipa mwanamume mwenye umri wa miaka 54, fidia ya Sh500,000 kwa kukosa kumbadilishia kitambulisho kilichopotea mwaka wa 1989.

Mahakama ya Mombasa pia iligundua kwamba Bw Abdul Mohammed Gulleid alishtakiwa kimakosa na serikali kwa madai ya kujisajili mara mbili alipotuma ombi la kupewa kitambulisho.

Jaji Eric Ogola alisema haki za Bw Gulleid zilikiukwa afisi ya msajili ilipokosa kumbadilishia kitambulisho.

Mahakama pia iliagiza Msajili Mkuu wa Watu kumbadilishia mzee huyo kitambulisho jinsi alivyokuwa ameomba.

You can share this post!

Amerika yatoa ahadi kusaidia Joho kufufua uchumi wa kaunti...

Aliyeshtakiwa kwa kumjeruhi mmiliki wa mkahawa jijini kwa...