• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 5:50 AM
Mwenyekiti wa ‘Shamba la Mauti’ azikwa

Mwenyekiti wa ‘Shamba la Mauti’ azikwa

NA MWANGI MUIRURI

ALIYEKUWA Mwenyekiti wa kampuni ya kununua na kuuza mashamba ya Embakasi Ranching James Njoroge amezikwa Jumanne katika shamba lake la Lironi katika eneobunge la Limuru, Kaunti ya Kiambu.

Marehemu Njoroge ameombolezwa, akitajwa kuwa mfanyabiashara ambaye dalili za bidii zilianza kudhihirika akiwa mwanafunzi ambapo shule zikifungwa alikuwa akichuuza mananasi.

Bidii yake ilimweka katika mkondo wa kupata mafanikio makuu maishani.

Alizaliwa mwaka wa 1954 katika Kaunti ya Kisii lakini Wakoloni wakafurusha familia yao hadi Kaunti ya Kiambu.

Mwendazake alisomea taaluma ya usimamizi hapa nchini na nchini Amerika na mwaka wa 1974 akajinunulia hisa katika shamba la Embakasi ambalo mwanzilishi alikuwa Hayati Mzee Jomo Kenyatta.

Aliteuliwa kuwa meneja wa kampuni hiyo na mwaka wa 2019 akachaguliwa kuwa mwenyekiti.

Agosti 26, 2023, Bw Njoroge aliaga dunia na ripoti ya upasuaji ilionyesha kwamba alikumbwa na mshtuko wa moyo licha ya kutokuwa na historia ya kuugua.

Wandani wake walidai kwamba matatizo yake ya kiafya yalimjia ghafla baada ya kuhudhuria mikutano na madalali wa sekta ya mashamba walio na mitandao na watu wenye ushawishi serikalini.

Wenyehisa wa Embakasi Ranching wamemtaka Rais William Ruto atumie kipindi cha mwezi mmoja kusaidia kuondoa taka na mkorogo kwenye mchakato wa kupeana hatimiliki kwa wamiliki halali.

La sivyo, wametishia kwamba watafanya maandamano na kufunga barabara kadhaa jijini Nairobi.

Diwani wa Ruai James Kariuki amesema wameshamweleza Rais Ruto tatizo lao kuhusu Embakasi Ranching.

“Tumemwambia Rais kuna tatizo Embakasi Ranching. Binafsi nimeshamweleza na mwenyewe amekubali kuna tatizo. Sasa ni lazima ajitokeze wazi kusaidia kuleta suluhiso,” Bw Kariuki amesema.

Diwani huyo amesema wako tayari kufa wakitetea na kulinda maslahi ya wamiliki halisi.

Alizaliwa mwaka wa 1954 katika Kaunti ya Kisii lakini Wakoloni wakafurusha familia yao hadi Kaunti ya Kiambu.

  • Tags

You can share this post!

Polisi wafungiwa ndani ya nyumba ya mshukiwa wa kuuza...

Vijana wa jamii ya Wapemba washauriwa kujaribu bahati yao...

T L