• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 5:50 AM
Vijana wa jamii ya Wapemba washauriwa kujaribu bahati yao jeshini

Vijana wa jamii ya Wapemba washauriwa kujaribu bahati yao jeshini

NA MAUREEN ONGALA

VIJANA kutoka kwa jamii ya Wapemba katika eneo la Pwani wameshauriwa kujitokeza na kushiriki katika zoezi la usajili wa makurutu ambalo linaendelea katika sehemu mbalimbali nchini.

Kulingana na afisa mkuu anayesimamia usajili wa makurutu wa jeshi la Kenya (KDF) katika uwanja wa Karisa Maitha mjini Kilifi Luteni Kanali Morris Nyaga, huenda vijana kutoka jamii hiyo wakapata nafasi hizo za ajira iwapo watajitokeza na stakabadhi zote zinazohitajika, pamoja na kukidhi viwango vingine vinavyohitajika.

Akizungumza na wanahabari mjini Kilifi wakati wa usajili huo wa makurutu, ameelezea kuwepo kwa idadi kubwa ya vijana ambao wamejitokeza kujaribu bahati yao, jambo ambalo anasema limechangiwa na suala la mji wa Kilifi kuwa na idadi kubwa ya Wakenya hasa vijana.

“Zoezi hili linalenga vijana kutoka divisheni za Bahari na Mastangoni ambazo zina makabila tofauti na ikiwa watajitokeza (Wapemba), watakuwa na nafasi nzuri ya kuchaguliwa pia,” akasema.

  • Tags

You can share this post!

Mwenyekiti wa ‘Shamba la Mauti’ azikwa

Salasya akwepa swali kuhusu mabadiliko ya tabianchi

T L