• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 8:55 PM
NCIC yachunguza kisa cha Wanjigi kupigwa mawe alipozuru Migori

NCIC yachunguza kisa cha Wanjigi kupigwa mawe alipozuru Migori

Na WINNIE ONYANDO

TUME ya Uwiano na Utangamano (NCIC), inachunguza kisa ambapo mwanasiasa wa Chama cha ODM, Jimi Wanjigi alipigwa mawe alipozuru Kaunti ya Migori.

Mwenyekiti wa Tume hiyo, Dkt Samuel Kobia, alisema vijana hao lazima wachukuliwe hatua ili iwe funzo kwa watu wanaotoa matamshi ya kuchochea chuki na ukabila nchini.

Akizungumza Jumatatu jijini Nairobi, Dkt Kobia alisema visa kama hivyo sharti vikomeshwe.

“Kisa cha Bw Wanjigi si cha kwanza. Tumevishuhudia visa vingi. Lazima visa kama hivyo vikomeshwe nchini,” akasema Dkt Kobia.

Alisema wanasisa wanawatumia vijana hasa waendeshaji bodaboda kuwavuruga washindani wao baada ya kuwahonga.

Kadhalika, alisema kuwa ofisi yake pia inaendelea kuchunguza visa ambavyo watu wanatumia mitandao ya kijamii kuendeleza ukabila, siasa na chuki.

“Sasa hivi tuna kesi zaidi ya 70 zinazohusishwa na matumizi ya mtandao wa kijamii kwa njia ya kuleta chuki kisiasa. Watu kama hao watachukuliwa hatua wakikamatwa,” akaongeza Dkt Kobia.

You can share this post!

Maafisa wanne wa polisi wanaoshtakiwa kwa mauaji ya wakili...

OCPD apumzishwa kwa heshima zote