• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 5:50 AM
Nimeolewa mke wa pili lakini mume hanidekezi hata

Nimeolewa mke wa pili lakini mume hanidekezi hata

SHANGAZI AKUJIBU:

Nimeolewa mke wa pili na mume wangu anagharamia mahitaji yote ya nyumbani. Hata hivyo, mara nyingi huwa na mkewe wa kwanza na humaliza hata mwezi bila kunitembelea. Ninaumia, nishauri.

Tabia ya mume wako inaonyesha hakuwa na mpango wa kuoa mke wa pili. Unajihadaa eti umeolewa ilhali unaumia kwa upweke. Ningekuwa wewe ningetoka katika ndoa hiyo nitafute mume.

Nina miaka 53, naye umri wake 30 na mbio zake chumbani zanilemea

Nina miaka 53. Sijaoa ingawa nimekuwa na wapenzi kadhaa. Niliye naye sasa ni mwanamke wa miaka 30. Nampenda lakini mbio zake chumbani zinanishinda. Naomba ushauri.

Huwezi kubadilisha hali hiyo. Wewe ni mzee na umeshiriki mbio hizo kwa miaka mingi. Naye mpenzi wako ni mchanga na huenda wewe ndiye wake wa kwanza. Mwambie ukweli ili muachane akatafute mtu wa ligi yake.

Safari zake za kazi kila mara zanitia dukuduku

Nimeolewa, niko na watoto watatu. Siku za hivi karibuni mzee amekuwa akisafiri kikazi karibu kila mwezi. Sijui kama kweli ni kazi ama ana mambo mengine. Nina shaka.

Wasiwasi wako ni kwamba huenda mumeo anakuhadaa anaenda kazini, lakini anatembea nje ya ndoa. Unaweza kujua ukweli tu huko kazini uwaulize wafanyakazi wenzake ama bosi wake.

Mama watoto anapeleka pesa za mahitaji kwingine

Nina mke na watoto wawili. Ninashuku mama watoto anatumia pesa za mahitaji ya nyumbani kwa mambo mengine. Lakini amejitetea akidai ni bidhaa zimekuwa ghali. Nifanyeje?

Kauli ya mke wako ni ya kweli. Kila mtu analalamikia hali ngumu ya uchumi sababu ya kupanda kwa bei za bidhaa. Kama unamshuku, andamane naye madukani ili uthibitishe mwenyewe.

  • Tags

You can share this post!

Benki ya AfDB yaahidi kutoa Sh3.6bn kusaidia kukabiliana na...

Ursula von der Leyen aahidi Afrika sapoti ya Ulaya...

T L