• Nairobi
  • Last Updated May 10th, 2024 8:50 AM
Pasta ashtakiwa kujeruhi mwanamke nyeti akimuombea

Pasta ashtakiwa kujeruhi mwanamke nyeti akimuombea

MCHUNGAJI anayedaiwa kuingiza mkono wake sehemu za siri za mwanamke mgonjwa akidai kumfanyia “maombi ya uponyaji” ameshtakiwa kwa kumsababishia madhara.

Mshukiwa anadaiwa kufanya kitendo hicho katika mtaa wa mabanda wa Mukuru kwa Njenga, Kaunti ya Nairobi.

Daniel Muriithi Njiru, anayehudumu katika kanisa la Only Believe Church of God Power of the Holy Spirit, anatuhumiwa kwa kumjeruhi vibaya mwanamke mwenye umri wa miaka 62 Jumanne wakati wa maombi.

Bw Njiru alikamatwa katika nyumba yake akimwombea mwathiriwa aliyekuwa akivunja damu.

Mwanamke huyo amekuwa akiugua kwa miaka mitatu iliyopita akipata shida ya kwenda haja kubwa.

Inadaiwa aliingiza mkono wake katika nyeti za mgonjwa ili “kuzifungua”.

Mwanamke huyo aliokolewa baada ya wakazi kuwaita polisi, kufuatia kilio kingi akitaka usaidizi.

Mwathiriwa amekuwa akienda katika hospitali kadhaa kupata tiba ya tatizo lake bila mafanikio.

Aliletwa jijini Nairobi na mwanawe ambaye baadaye alimpeleka katika nyumba ya mhubiri huyo ili kufanyiwa sala ya uponyaji.

Alipelekwa kwa nyumba ya Bw Njiru tangu mwezi uliopita kuhudhuria maombi hayo hadi Julai 31 wakati mshukiwa alimrai kubakia naye kwa muda wa wiki moja.

Mwathiriwa alikuwa amekaa hapo kwa siku mbili akiombewa huku mchungaji huyo akidai kuwa angemponya katika muda huo wa juma moja.

Baada ya kuokolewa mwanamke huyo alipelekwa katika hospitali ya Mama Lucy Kibaki eneo la Embakasi ambako amelazwa.

Mshukiwa alikana mashtaka mbele ya Hakimu Mkuu Irene Gichobi.

Aliachiliwa kwa bondi ya Sh50,000 taslimu ama mdhamini wa Sh100,000.

  • Tags

You can share this post!

Aliyekuwa wakili wa Ruto ICC atuzwa shahada Kenya

Masharti makali ya Azimio kwa Kenya Kwanza

T L