• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 6:21 PM
Polisi 6 wakanusha mauaji ya ndugu wawili wa Kianjokoma

Polisi 6 wakanusha mauaji ya ndugu wawili wa Kianjokoma

Na RICHARD MUNGUTI

JUHUDI za polisi sita kutaka wasishtakiwe kwa mauaji ya ndugu wawili kaunti ya Embu mnamo Agosti 1, 2021 ziligonga mwamba jana Mahakama Kuu ilipotupilia mbali maombi matatu ya kufutilia mbali kesi hiyo.

Akikataa ombi la maafisa hao sita kupinga wasifunguliwe mashtaka ya mauaji ya Emmanuel Mutura Ndwiga na Benson Njiru, Jaji Daniel Ogembo alisema suala la vifo vya wavulana hao lina uzito wa kitaifa na limeteka hisia za wananchi wote.

Jaji Ogembo alisema lazima haki itendeke na endapo washtakiwa hao wana ushahidi kwamba hawakuhusika na mauaji ya ndugu hao, bila shaka mahakama itawaachilia huru.

Jaji huyo alisema tangu Agosti 14, 2021 maafisa hao waliwasilisha maombi matatu ya kupinga kushtakiwa kwa mauaji ya Njiru na Mutura, na badala yake mahakama iamuru uchunguzi wa kubaini kilichosababisha vifo hivyo ufanywe.

Maafisa hao wa polisi Koplo Corporal Benson Mbuthia Mabuuri, Koplo Consolata Njeri Kariuki,Martin Musamali Wanyama, Nicholas Sang Cheruiyot, Lilian Cherono Chemuna na James Mwaniki Njohu waliwasilisha maombi matatu mbele ya Jaji Ogembo na Jaji Weldon Korir wakiomba mashtaka dhidi yao kupigwa breki na badala yake mahakama kuu iagize uchunguzi kubaini kilichosababisha vifo vya Mutura na Njiru ufanywe.

Akiwasilisha maombi hao wakili wao Bw Dunstan Omari alimweleza Jaji Ogembo kuwa sheria nambari 386 na 387 zimeamuru uchunguzi wa kubaini kilichosababisha kifo cha mshukiwa anayekata roho akiwa aidha mikononi mwa polisi ama mikononi kwa askari jela ama anapozuiliwa gerezani.

Katika ushahidi aliowasilisha mbele ya Majaji Ogembo na Korir, Bw Omari alisema wahasiriwa waliruka kutoka kwa gari la polisi na kuanguka na kufa papo hapo.

You can share this post!

Yaibuka Ruto aligawia Jumwa GSU wawili ilhali ana kesi

Vihiga Queens wajikatia tiketi ya kulimana na Simba Queens