• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 2:31 PM
Sakaja apata shavu mpango wa ‘Dishi na County’ ukijadiliwa nchini Ufaransa

Sakaja apata shavu mpango wa ‘Dishi na County’ ukijadiliwa nchini Ufaransa

NA WINNIE ONYANDO

GAVANA wa Nairobi Johnson Sakaja ndiye aliyemwakilisha Rais William Ruto katika Kongamano kuhusu Lishe Shuleni linalofanyika nchini Ufaransa.

Mkutano huo unawaleta pamoja viongozi mbalimbali wakiwemo marais na mawaziri.

Kiini cha mkutano huo ni kutoa changamoto kwa nchi mbalimbali kuwekeza katika mfumo endelevu wa lishe kupitia mpango kama vile lishe shuleni.

Gavana huyo ameiwakilisha nchi kwenye mkutano huo na anatarajiwa kuzungumzia kuhusu programu yake ya ‘Dishi na County’ iliyozinduliwa Agosti 2023.

“Watoto wetu wanafaa kufahamu kuwa serikali huwajali,” gavana Sakaja alisema akiwa jijini Paris.

Programu hiyo ya gavana Sakaja imekuwa ikikashifiwa huku baadhi ya watu wakitilia shaka utekelezaji wake.

Hata hivyo, Sakaja amekuwa akiutetea mpango huo akisema kuwa watu wanaoupinga mpango wana nia fiche.

“Hakuna haja kuendeleza propaganda. Kadhalika, hakuna haja kuwatumia watoto kuendeleza ajenda za kisiasa. Shule ambazo zilikuwa katika orodha ya awamu ya kwanza zimekuwa zikipokea chakula kila siku bila kuchelewa. Tayari, watoto 80,000 wanapata chakula chini ya programu hiyo,” Sakaja alisema.

Mpango wa ‘Dishi na County’ unanuia kuwafaa wanafunzi 250,000 katika shule zote za umma jijini Nairobi.

  • Tags

You can share this post!

Kilio cha wahasiriwa wa ubomoaji nyumba Mavoko chageuzwa...

Pesa zaleta mpasuko katika Baraza la Wazee wa Njuri Ncheke

T L