• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 12:48 PM
Sampuli za wanaohofiwa kuugua ‘monkeypox’ kupimwa nchini Senegal

Sampuli za wanaohofiwa kuugua ‘monkeypox’ kupimwa nchini Senegal

NA ANGELA OKETCH

SAMPULI za Wakenya wanne wanaohofiwa kuugua ugonjwa wa ndui ya nyani jana zilisafirishwa hadi Senegal kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu.

Wizara ya Afya jana Ijumaa iliidhinisha sampuli hizo zipimwe katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi kwa sababu Kenya haina vifaa vya kuendesha vipimo hivyo kwa ugonjwa huo ambao ni nadra sana uchipuke.

“Vipimo hivyo vinatumika na kemikali na kwa kuwa hatuna uwezo na rasilimali ya kuendesha vipimo hivyo, ilibidi tuwapeleke hadi nchi ambayo imepambana na virusi hivyo na maabara yao yameidhinishwa,” akasema afisa wa wizara ya afya.

Waziri wa Afya, Mutahi Kagwe na Katibu Susan Mochache hawakupokea simu za Taifa Leo ili kuzungumzia suala hilo.

Kaimu Mkuu wa Idara inayohusika na kutathmini maambukizi ya magonjwa Dkt Emmanuel Okunga naye alisema nchi imekuwa na kisa kimoja tu kinachoshukiwa cha mtu kuugua ndui ya nyani.

Hata hivyo, alisema vipimo vilionyesha mtu aliyeshukiwa kuugua ugonjwa huo hakua nao.

Wakati huo huo, Wakenya ambao walipokea chanjo ya corona miezi sita iliyopita wameshauriwa waendee dozi ya nne ili kuimarisha kinga dhidi ya corona mwilini mwao wakati ambapo maambukizi yamekuwa yakiongezeka nchini.

Wataalamu hao wakiongozwa na Dkt Ahmed Kalebi walisema kupokea dozi ya nne kutadidimiza zaidi uwezekano wa raia kuambukizwa virusi vya corona.

  • Tags

You can share this post!

Jinsi mitihani ya CBC kwa Gredi 6 itakavyotolewa

Uholanzi wapepeta Ubelgiji katika Uefa Nations League

T L