• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 12:48 PM
Ufisadi: Ruto aagiza maafisa 29 wa huduma za misitu wafutwe kazi

Ufisadi: Ruto aagiza maafisa 29 wa huduma za misitu wafutwe kazi

NA JOSEPH OPENDA

RAIS William Ruto ameamuru maafisa 29 wa Shirika la Huduma za Misitu Nchini (KFS), waliohusishwa na shughuli za ufisadi na uharibifu wa rasilimali za misitu nchini wafutwe kazi na kufunguliwa mashtaka.

Dkt Ruto alisema utawala wake hautaunga mkono ufisadi katika sekta za uhifadhi wa misitu na maji. “Hatutaruhusu watu wachache wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu kutunyima fursa ya kufurahia bidii yetu ya kuhifadhi msitu,” alisema.

Aliongeza, “Kuna wasimamizi na maafisa wa misitu 29 ambao tayari wamepatikana na hatia. Naagiza bodi ya KFS kuwafuta na kuwaondoa kwenye orodha ya malipo wale wote watakaopatikana na hatia ya kuendeleza ufisadi katika sekta hiyo.”

“Kuanzia kesho, siwataki kwenye orodha ya malipo ya serikali kwa kuwa ni wahujumu wanaoendeleza uharibifu wa mazingira yetu,” akaongeza Dkt Ruto.

Rais alisema serikali yake itachukua hatua zote kulinda misitu na kuhakikisha maafisa walio na uadilifu wanaendelea kuhudumu.

  • Tags

You can share this post!

Mbinu faafu za kilimo zaletea wakulima afueni

Israel yasema wanajeshi wake 169 wameangamia huku...

T L