• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 3:46 PM
Israel yasema wanajeshi wake 169 wameangamia huku wakiendelea kunyeshea makombora Gaza

Israel yasema wanajeshi wake 169 wameangamia huku wakiendelea kunyeshea makombora Gaza

JERUSALEM, Israeli

Na AFP

WANAJESHI 169 wa Israeli wameuawa katika mapigano dhidi ya kundi la wapiganaji wa Kipalestina, Hamas, jeshi la Israeli (IDF) lilisema jana.

Vita hivyo vilianza Jumamosi wiki jana baada ya wapiganaji hao wa Kiislamu kutekeleza mashambulio kadha ya roketi ndani ya Israeli.

“Kufikia leo asubuhi, tumeziarifu familia za wanajeshi wetu 169 waliouawa katika vita dhidi ya Hamas,” msemaji wa IDF Daniel Hagari aliwaambia wanahabari.

Aliongeza kuwa familia za watu 60 waliotekwa na kupelekwa eneo la Gaza pia zimepashwa habari.

Moshi wafuka kutokana na mashambulizi ya Israeli katika Ukanda wa Gaza, nchini Palestina huku uhasama ukichacha. Picha|AFP

Licha ya hayo, wanajeshi wa Israeli jana waliendelea kushambulia vituo vya Hamas katika Ukanda wa Gaza ambapo majengo katika vitongoji mbalimbali yamegeuzwa vifusi.

Wanajeshi hao pia walipata miili zaidi ya waliouawa katika vita hivyo, siku tano baada ya wapiganaji wa Hamas kushambulia miji ya kusini mwa Israeli.

Jeshi la Israeli lilisema zaidi ya miili 1,200 imepatikana, mingi ikiwa ni ya raia wasio na silaha.

Hata hivyo, maafisa wa Gaza waliripoti kuwa zaidi ya watu 900 waliouawa katika mashambulio ya angani na ardhini, yaliyotekelezwa na Israeli, katika eneo hilo wanakoishi Wapalestina wengi.

Israeli imepeleka wanajeshi, mizinga na silaha zinginezo kubwa, katika Gaza kama sehemu ya kampeni zake za kulipiza kisasa kile ambacho Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu alitaja kama “shambulio la kishenzi zaidi kuwahi kufanywa dhidi ya Israeli na magaidi”.

Rais wa Amerika Joe Biden ameahidi kutuma silaha zaidi na vifaa vingine vya kivita kusaidia mshirika wake, Israeli, katika vita hivyo.

Amelaani mauaji ya raia kufuatia shambulio lililotekelezwa na Hamas dhidi ya Israeli Jumamosi wiki jana.

Hofu imetanda kuhusu kuhusu kuzuka changamoto kubwa ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza.

Hii ni baada ya Israeli kubomoa zaidi ya majengo 1,000 kukatiza huduma za usambazaji wa maji, umeme, chakula na mahitaji mengine ya kimsingi kwa zaidi ya wakazi 2.3 milioni eneo hilo.

Zaidi ya wakazi 260,000 wa Gaza wamelazimika kutoroka makwao, Umoja wa Mataifa (UN) imesema.

Kwa upande wake Umoja wa Ulaya (EU) umehimiza kutengwa kwa “mkondo wa kibinadamu” utakautumiwa na rais kutoroka mapigano haya yanapoendelea.

Israeli ilionekana kujiandaa kutekeleza uvamizi wa ardhini katika Gaza, lakini inakabiliwa na hatari ya kushambuliwa na mataifa mengine yanayounga mkono Hamas.

Hii ni baada ya taifa hilo kuzongwa na mashambulio ya roketi kutoka kwa makundi ya wapiganaji katika nchi jirani za Lebanon na Syria.

Hata hivyo, jana, Israeli ilishambulia vituo kadha kusini mwa Lebanon, eneo linalodhibitiwa na Hezbollah, mshirika wa hasidi wa Israeli, Iran.

Israeli imetikiswa zaidi na shambulio baya zaidi kuwahi kutekelezwa dhidi yake ndani ya miaka 75 na kufeli kwa idara yake ya ujasusi.

Ni kutokana na kufeli kwa idara yake ya ujasusi ambapo zaidi ya wapiganaji 1, 500 wa Hamas walivuka ua la usalama eneo la Gaza na kushambulia taifa hilo; kupitia angani, ardhini na majini.

  • Tags

You can share this post!

Ufisadi: Ruto aagiza maafisa 29 wa huduma za misitu wafutwe...

Mikakati ya serikali kuzima visa vya utekaji nyara nchini

T L