• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 7:12 PM
Uholanzi kushirikiana na Kenya kuibuka na aina ya viazi itakayostahimili athari za mabadiliko ya tabianchi

Uholanzi kushirikiana na Kenya kuibuka na aina ya viazi itakayostahimili athari za mabadiliko ya tabianchi

Na SAMMY WAWERU

UHOLANZI inaendelea kushirikiana na Kenya ili kuibuka na mbegu za viazimbatata ambavyo vitaweza kustahimili makali ya mabadiliko ya tabianchi.

Naibu Balozi wa Uholanzi hapa nchini Kenya, Bw Joris van Bommel amesema mikakati hiyo inatekelezwa na vyuo vikuu vya Uholanzi kwa ushirikiano na taasisi za utafiti wa kilimo Kenya.

Zinajumuisha Taasisi ya Utafiti wa Kilimo cha Mimea na Uimarishaji Mifugo (Karlo) na ile ya Mbegu na Ustawishaji wa Mimea (Kephis), pamoja na wadauhusika wengine katika sekta ya uzalishaji viazi.

“Huku tukiendeleza mipango kuboresha na kuongeza kiwango cha uzalishaji wa viazimbatata hapa nchini, tunajikakamua kuibuka na mbegu za kisasa za viazi ambavyo vitaweza kustahili makali ya mabadiliko ya tabianchi, kama vile athari za ukame, magonjwa na wadudu,” Bw Bommel akasema, akizungumza jijini Nairobi.

Naibu Balozi huyo ambaye pia ni Msimamizi wa Masuala ya Biashara na Maendeleo katika Ubalozi wa Uholanzi Kenya, alisema utafiti huo unaendeshwa kwa kutumia mifumo ya teknolojia ya kisasa.

Naibu Balozi wa Uholanzi hapa nchini Kenya, Bw Joris van Bommel asema Kenya na Uholanzi zinashirikiana kuibuka na mbegu za kisasa za viazimbatata vitakavyostahimili athari za mabadiliko ya tabianchi…PICHA/ SAMMY WAWERU

“Mabadiliko ya tabianchi yamejiri na athari zake, na ili taifa liwe na mazao ya kutosha ya viazi, tunahitaji kuwa na mbegu za hadhi ya juu,” akaelezea.Uholanzi ndiye mzalishaji mkuu wa mbegu za viazimbatata duniani.

Kenya imekuwa ikishirikiana na taifa hilo katika kuboresha uzalishaji wa viazi kwa zaidi ya miaka kumi. ‘

  • Tags

You can share this post!

Sheria ya watu fisadi kuepuka korti yatua bungeni

Vipusa wa Man-City na Chelsea kukutana kwenye nusu-fainali...