• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 10:15 PM
UNESCO kufanya ushirikiano na vyuo vikuu viwili nchini

UNESCO kufanya ushirikiano na vyuo vikuu viwili nchini

Na LAWRENCE ONGARO

SHIRIKA la UNESCO katika Afrika Mashariki na Kati lina umuhimu wake wa kujumuisha wanafunzi wa vyuo vikuu pamoja.

UNESCO kwa ushirikiano na Chuo Kikuu cha Mount Kenya (MKU) na kile cha Nairobi, imezindua mradi wa 03 Plus, ambao unalenga kuunda mtaala mpya utakaofuatwa kwenye masomo ya vyuo hivyo.

Mradi huo ulizinduliwa katika MKU, chuo chenye wanafunzi zaidi ya 1,500 kilichoko mjini Thika.

Naibu Chansela wa MKU Prof Deogratius Jaganyi, alisema kutokana na masomo yanayoendeshwa kimtandao, wanafunzi weñgi watanufaika pakubwa.

“Tunataka wanafunzi wanufaike na masomo yanayoendeshwa katika vyuo vikuu hivi viwili,” alisema Prof Jaganyi.

Alisema hata ingawa wanafunzi wote hawaishi ndani ya chuo hicho, lakini wengine hukodi nje ya chuo lakini wote wanapata masomo sawa.

“Hata ingawa wanafunzi wengi wamepitia changamoto nyingi, ukweli wa mambo ni kwamba mradi huo utakuwa pia wa kuwapa mwongozo wa kuwasaidia kupanga maisha yao katika siku zijazo,” alisema msomi huyo.

Prof Jaganyi alinukuu kauli ya aliyekuwa rais wa Afrika Kusini, kwamba, ‘Elimu ni silaha muhimu ya kugeuza ulimwengu’ huku akisema ni muhimu kufuata usemi huo.

Alisema kuna changamoto nyingi zinazoyumbisha maisha ya wanafunzi wengi vyuoni lakini wakiwa na mwelekeo mwema bila shaka watafuata mkondo unaostahili.

Alisema ushirikiano wa vyuo hivyo viwili pamoja na Shirika la UNESCO ni muhimu sana kwa kubadilishwa mwelekeo wa masomo kwa mtindo unaostahili.

Alisema hivi karibuni watafanya zoezi la matambezi mjini Thika na wanatarajia kualika UoN.

You can share this post!

KDF kusaidia kukabiliana na ukame

Mzozo wa Kalonzo, Mudavadi watishia kutawanya OKA