• Nairobi
  • Last Updated May 16th, 2024 8:50 PM
Vuguvugu la wahubiri 500 lataka Raila asitishe maandamano

Vuguvugu la wahubiri 500 lataka Raila asitishe maandamano

NA SAMMY KIMATU

WAHUBIRI zaidi ya 500 wamekosoa wito wa kinara wa Azimio la Umoja-One Kenya, Bw Raila Odinga wa kuwataka wafuasi wake kupinga uongozi wa Rais William Ruto kwa kuandamana kesho Jumatatu.

Wakiongozwa na mwenyekiti wao Askofu Dkt Josphat Njoroge, Sauti Mashinani Ministries Movement wamerai Wakenya waende kazini Jumatatu badala ya kuenda barabarani kuandamana.

Aidha, wamesema maandamano hayo yatachangia kusambaratika kwa biashara jambo litakalochangia zaidi uchumi kuzoroteka.

Walisema badala ya kuandamana, Bw Raila atafute njia mbadala ya kusuluhisha tofauti zake na Bw Ruto wakihofia umwagikaji wa damu na mali kuporwa.

“Raila ampatie rais nafasi ya kuongoza serikali. Tunataka maafisa wa polisi kuweka ulinzi mkali ndiposa wanafunzi wapate nafasi ya kurudi shuleni baada ya kumaliza likizo fupi ya muhula wa kwanza. Hatutaki kuona fujo zilizokuwa baada ya uchaguzi mwaka 2007/2008 hapa nchini,” Askofu Njoroge akahoji.

Mhubiri huyo, amezungumza Jumapili akiwa ameongoza wenzake katika mkutano na wanahabari uliofanyika katika kanisa la Jesus Restoration katika mtaa wa Njiru.

  • Tags

You can share this post!

Raila: Mambo yako hivi…

UJASIRIAMALI: Jinsi wazo la kutatua changamoto ya kiafya...

T L