• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 10:50 AM
Wabunge kujadili hatua ya TSC kuadhibu walimu waliokataa uhamisho hadi maeneo hatari

Wabunge kujadili hatua ya TSC kuadhibu walimu waliokataa uhamisho hadi maeneo hatari

DAVID MUCHUNGUH na MERCY SIMIYU

WABUNGE wiki ijayo watajadiliana na Tume ya Kuajiri Walimu (TSC) kuhusu mstakabali wa walimu 129 walioadhibiwa kwa kukata agizo la kuwataka kuhamia maeneo ya Kaskazini Mashariki wakihofia maisha yao kwa sababu ya mashambulio ya mara kwa mara.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge kuhusu Elimu, Julius Melly, alitangaza hayo Ijumaa baada ya kuwasikiliza walimu hao katika ukumbi wa County Hall.

Mkutano huo utafanyika Jumanne kukwamua mkwamo ulioko baada ya walimu hao kutaka wapelekwe kwingineko.

“Mtu akiwa hayuko salama, humuadhibu bali unamlinda. Tutaisikiliza TSC ili njia bora ya kuwafaa walimu ipatikane,” akasema Bw Melly.

Ingawa hivyo, alisema serikali haiwezi ikahamisha walimu wote 3,200 ambao si wenyeji lakini wale walio katika hatari kubwa wanafaa kuhamishwa.

Kwa upande wake Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu, aliwataka walimu kurudi kwa maeneo yao ya kazi, akisisitiza usalama umeimarika katika kaunti za Garissa, Wajir na Mandera.

Walimu waliambia wabunge kwamba mara nyingi hushambuliwa kwa sababu si wenyeji wa maeneo hayo.

Pia walidai wenyeji wa maeneo hayo nao huwabagua kwa msingi wa kidini na kikabila.

“Niko tayari kufanya kazi katika eneo lolote la nchi mradi tu nihakikishiwe usalama lakini si katika eneo la Kaskazini Mashariki,” alisema Charles Achol ambaye alisoma malalamiko kwa niaba ya walimu hao.

  • Tags

You can share this post!

Vuguvugu lafika kortini kupiga breki hatua yoyote ya Bunge...

Jinsi chai ilivyosababisha mkanyagano na vifo Kericho

T L